10
Mataifa Yaliyotokana Na Noa
(1 Nyakati 1:5-23)
Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.
Wazao Wa Yafethi
Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
Wana wa Yavani walikuwa:
Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)
Wazao Wa Hamu
Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misraimu,* Putu na Kanaani.
Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
 
Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 11 Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, 12 na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
 
13 Misraimu alikuwa baba wa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 14 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15 Kanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17 Wahivi, Waariki, Wasini, 18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
 
Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
20 Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Wazao Wa Shemu
21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.
 
22 Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23 Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
24 Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.
25 Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
26 Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27 Hadoramu, Uzali, Dikla, 28 Obali, Abimaeli, Sheba, 29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
 
30 Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.
31 Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
 
32 Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
* 10:6 Yaani Misri.