12
Orodha Ya Wafalme Walioshindwa
1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:
2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.
4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6 Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
8 nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):
9 mfalme wa Yeriko | mmoja |
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) | mmoja |
10 mfalme wa Yerusalemu | mmoja |
mfalme wa Hebroni | mmoja |
11 mfalme wa Yarmuthi | mmoja |
mfalme wa Lakishi | mmoja |
12 mfalme wa Egloni | mmoja |
mfalme wa Gezeri | mmoja |
13 mfalme wa Debiri | mmoja |
mfalme wa Gederi | mmoja |
14 mfalme wa Horma | mmoja |
mfalme wa Aradi | mmoja |
15 mfalme wa Libna | mmoja |
mfalme wa Adulamu | mmoja |
16 mfalme wa Makeda | mmoja |
mfalme wa Betheli | mmoja |
17 mfalme wa Tapua | mmoja |
mfalme wa Heferi | mmoja |
18 mfalme wa Afeki | mmoja |
mfalme wa Lasharoni | mmoja |
19 mfalme wa Madoni | mmoja |
mfalme wa Hazori | mmoja |
20 mfalme wa Shimron-Meroni | mmoja |
mfalme wa Akishafu | mmoja |
21 mfalme wa Taanaki | mmoja |
mfalme wa Megido | mmoja |
22 mfalme wa Kedeshi | mmoja |
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli | mmoja |
23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) | mmoja |
mfalme wa Goimu katika Gilgali | mmoja |
24 mfalme wa Tirsa | mmoja |
wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.