8
Ukoo Wa Sauli Mbenyamini
Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,
Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,
Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
Wana wa Bela walikuwa:
Adari, Gera, Abihudi, Abishua, Naamani, Ahoa, Gera, Shefufani na Huramu.
Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara. Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. 11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
12 Wana wa Elpaali walikuwa:
Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka), 13 na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15 Zebadia, Aradi, Ederi, 16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
19 Yakimu, Zikri, Zabdi, 20 Elienai, Silethai, Elieli, 21 Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, 23 Abdoni, Zikri, Hanani, 24 Hanania, Elamu, Anthothiya, 25 Ifdeya na Penueli.
26 Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27 Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
28 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.
 
29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.
Mke wake aliitwa Maaka. 30 Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 31 Gedori, Ahio, Zekeri, 32 na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
34 Yonathani akamzaa:
Merib-Baali,* naye Merib-Baali akamzaa Mika.
35 Wana wa Mika walikuwa:
Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.
36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 37 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:
Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.
39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:
Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.
Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.
 
* 8:34 Merib-Baali maana yake ni Baali na Ashindane naye (Amu 6:32); ni jina lingine la mwana wa Yonathani, Mefiboshethi ambalo nalo maana yake ni Mtu wa Aibu (ona 2Sam 4:4).