10
Mimi Paulo, mwenyewe nawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo. Mimi ni mpole wakati nikiwa mbele yenu, Lakini ninaujasiri kwenu wakati nikiwa mbali nanyi. Nawaomba ninyi kwamba, wakati nikiwepo pamoja nanyi, sitahitaji kuwa jasiri na kujiamini kwangu mwenyewe. Lakini nafikiri nitahitaji kuwa jasiri wakati nikiwapinga wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa jinsi ya mwili. Kwa kuwa hata kama tunatembea katika mwili, hatupigani vita kwa jinsi ya mwili. Kwa kuwa silaha tunazotumia kupigana si za kimwili. Badala yake, zina nguvu ya kiungu ya kuharibu ngome. Zinaondosha kabisa mijadara inayopotosha. Pia, tunaharibu kila chenye mamlaka kijiinuacho dhidi ya maarifa ya Mungu. Tunalifanya mateka kila wazo katika utii kwa Kristo. Na tunapata utayari wa kuadhibu kila matendo lisilo na utii, mara tu utii wenu unapokuwa kamili. Tazama kile kilichowazi mbele yenu. Kama yeyote anashawishika kwamba yeye ni wa Kristo, na hebu ajikumbushe yeye mwenyewe kwamba kama tu alivyo ni wa Kristo, hivyo ndiyo na sisi pia tuko hivyo. Kwa kuwa hata nikijivuna kidogo zaidi kuhusu mamlaka yetu, ambayo Bwana aliyatoa kwa ajili yetu kuwajenga ninyi na siyo kuwaharibu, sitaona haya. Sihitaji hili lionekane kwamba nawatisha ninyi kwa nyaraka zangu. 10 Kwa vile baadhi ya watu husema, “ Nyaraka zake ni kali na zina nguvu, lakini kimwili yeye ni dhaifu. Maneno yake hayastahili kusikilizwa.” 11 Hebu watu wa jinsi hiyo waelewe kwamba kile tusemacho kwa waraka wakati tukiwa mbali, ni sawasawa na vile tutakavyotenda wakati tukiwa pale. 12 Hatuendi mbali mno kama kujikusanya wenyewe au kujilinganisha wenyewe na wale ambao hujisifia wenyewe. Lakini wanapojipima wenyewe na kila mmoja wao, hawana akili. 13 Sisi, hata hivyo, hatutajivuna kupita mipaka. Badala yake, tutafanya hivyo tu ndani ya mipaka ambayo Mungu ametupimia sisi, mipaka inayofika umbali kama wenu ulivyo. 14 Kwa kuwa hatukujizidishia wenyewe tulipowafikia ninyi. Tulikuwa wa kwanza kufika kwa umbali kama wenu kwa injili ya Kristo. 15 Hatujajivuna kupita mipaka kuhusu kazi za wengine. Badala yake, tunatumaini kama imani yenu ikuwavyo kwamba eneo letu la kazi litapanuliwa sana, na bado ni ndani ya mipaka sahihi. 16 Tunatumaini kwa hili, ili kwamba tuweze kuhubiri injili hata kwenye mikoa zaidi yenu. Hatutajivuna kuhusu kazi inayofanywa katika maeneo mengine. 17 “Lakini yeyote ajivunaye, ajivune katika Bwana.” 18 Kwa maana siyo yule ajithibitishaye mwenyewe anathibitishwa. Isipokuwa, ni yule ambaye Bwana humthibitisha.