3
Je, tumeanza kujisifia wenyewe tena? Hatuhitaji barua ya mapendekezo kwenu au kutoka kwenu, kama baadhi ya watu, je twahitaji? Ninyi wenyewe ni barua yetu ya mapendekezo, iliyoandikwa kwenye mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na watu wote. Na mnaonesha kwamba ninyi ni barua kutoka kwa Kristo, iliyotolewa na sisi. Iliandikwa siyo kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu. Na huu ndiyo ujasiri tulio nao katika Mungu kupitia Kristo. Hatujiamini wenyewe kwa kudai chochote kama kutoka kwetu. Badala yake, kujiamini kwetu kunatoka kwa Mungu. Ni Mungu ambaye alitufanya tuweze kuwa watumishi wa agano jipya. Hili ni agano sio la barua bali ni la Roho. Kwa kuwa barua huua, lakini roho inatoa uhai. Sasa kazi ya kifo iliyokuwa imechongwa katika herufi juu ya mawe ilikuja kwa namna ya utukufu kwamba watu wa Israeli hawakuangalia moja kwa moja kwenye uso wa Musa. Hii ni kwa sababu ya utukufu wa uso wake, utukufu ambao ulikuwa unafifia. Je, kazi ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? Kwa kuwa kama huduma ya hukumu ilikuwa na utukufu, ni mara ngapi zaidi huduma ya haki huzidi sana katika utukufu! 10 Ni kweli kwamba, kile kilichofanywa utukufu kwanza hakina utukufu tena katika heshima hii, kwa sababu ya utukufu unaouzidi. 11 Kwa kuwa kama kile ambacho kilikuwa kinapita kilikuwa na utukufu, ni kwa kiasi gani zaidi kile ambacho ni cha kudumu kitakuwa na utukufu! 12 Kwa kuwa tunajiamini hiyo, tunaujasiri sana. 13 Hatuko kama Musa, aliyeweka utaji juu ya uso wake, ili kwamba watu wa Israel wasiweze kuangalia moja kwa moja kwenye mwisho wa utukufu ambao ulikuwa unatoweka. 14 Lakini fahamu zao zilikuwa zimefungwa. Hata mpaka siku hii utaji uleule bado unabaki juu ya usomaji wa agano la kale. Haijawekwa wazi, kwa sababu ni katika Kristo pekee inaondolewa mbali. 15 Lakini hata leo, wakati wowote Musa asomwapo, utaji hukaa juu ya mioyo yao. 16 Lakini mtu anapogeuka kwa Bwana, utaji unaondolewa. 17 Sasa Bwana ni Roho. Palipo na Roho wa Bwana, kuna uhuru. 18 Sasa sisi sote, pamoja na nyuso zisizo wekewa utaji, huona utukufu wa Bwana. Tunabadilishwa ndani ya muonekano uleule wa utukufu kutoka shahada moja ya utukufu kwenda nyingine, kama ilivyo kutoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.