5
Tunajua kwamba kama maskani ya ulimwenguni ambayo tunaishi humo yanaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu. Ni nyumba isiyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, bali ni nyumba ya milele, katika mbingu. Kwa kuwa katika hema hii tunaugua, tukitamani kuvikwa kwa maskani yetu mbinguni. Tunatamani kwa ajili ya hii kwa sababu kwa kuivaa hatutaonekana kuwa tu uchi. Kwa hakika wakati tuko ndani ya hema hii, twaugua tukilemewa. Hatutaki kuvuliwa. Badala yake, tunataka kuvalishwa, ili kwamba kile kilicho kufa kiweze kumezwa na uzima. Yule aliyetuandaa sisi kwa kitu hiki ni Mungu, ambaye alitupa sisi Roho kama ahadi ya kile kitakacho kuja. Kwa hiyo muwe na ujasiri siku zote. Muwe macho kwamba wakati tuko nyumbani katika mwili, tuko mbali na Bwana. Kwa kuwa tunatembea kwa imani, sio kwa kuona. Kwa hiyo tunaujasiri. Ni bora tuwe mbali kutoka kwenye mwili na nyumbani pamoja na Bwana. Kwa hiyo tunaifanya kuwa lengo letu, kama tukiwa nyumbani au mbali, tumpendeze yeye. 10 Kwa kuwa lazima wote tuonekane mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kwamba kila mmoja aweze kupokea kile kinachostahili kwa mambo yaliyofanyika katika mwili, ikiwa ni kwa uzuri au kwa ubaya. 11 Kwa hiyo, kwa kuijua hofu ya Bwana, tunawashawishi watu. Jinsi tulivyo, inaonekana wazi na Mungu. Ninatumaini kuwa inaeleweka pia kwenye dhamiri zenu. 12 Hatujaribu kuwashawishi ninyi tena kutuona sisi kama wakweli. Badala yake, tunawapa ninyi sababu ya kujivuna kwa ajili yetu, ili kwamba muweze kuwa na jibu kwa wale wanaojivunia kuhusu mwonekano lakini sio kile kilicho ndani ya moyo. 13 Kwa kuwa ikiwa kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu. Na kama tuko kwenye akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu. 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo watushurutisha, kwa sababu tuna uhakika na hili: kuwa mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote, na kwa hiyo wote wamekufa. 15 Na Kristo alikufa kwa ajili ya wote, ili kwamba wale wanaoishi wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe. Badala yake, lazima waishi kwa ajili yake yeye ambaye alikufa na alifufuliwa. 16 Kwa sababu hii, kuanzia sasa na kuendelea hatumuhukumu mtu kulingana na viwango vya wanadamu, ingawa hapo kwanza tulimtazama Kristo katika namna hii. Lakini sasa hatumuhukumu yeyote kwa namna hii tena. 17 Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya. 18 Vitu vyote hivi vyatoka kwa Mungu. Alitupatanisha sisi kwake mwenyewe kupitia Kristo, na ametupatia huduma ya upatanisho. 19 Hiyo ni kusema, katika Kristo, Mungu anaupatanisha ulimwengu kwake mwenyewe, sio kuhesabu makosa yao dhidi yao. Anawekeza kwetu ujumbe wa upatanisho. 20 Kwa hiyo tunateuliwa kama wawakilishi wa Kristo, kana kwamba Mungu alikuwa anafanya rufaa yake kupitia sisi. Tunawasihi ninyi kwa ajili ya Kristo: “Mpatanishwe kwa Mungu!” 21 Alimfanya Kristo kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye ndiye ambaye hakutenda dhambi. Alifanya hivi ili tuweze kufanyika haki ya Mungu katika yeye.