26
1 Hivyo ilikuwa katika mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema juu ya Yerusalemuu, 'Aha! Malango ya watu waliovunjika! Amenigeukia; Nitajazwa kwa sababu ameharibika.'
3 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama! Niko juu yako, Tiro, na nitayainua mataifa mengi juu yako kama bahari iiunuavyo mawimbi yake.
4 Wataziharibu kuta za Tiro na kuiangusha chini minara yao. Nitafagia mavumbi yake mbali na kumfanya kama jiwe tupu.
5 Atakuwa sehemu ya kuwekea nyavu kati ya bahari, kwa kuwa nimesema hilo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na atakuwa mateka kwa ajili ya mataifa.
6 Binti zake walioko mashambani watachinjwa kwa panga, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.'
7 Kwa kuwa hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Tazama, kutoka kaskazini namleta Nebukadreza mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, dhidi ya Tiro, pamoja na farasi na magari ya farasi, na pamoja na waendesha farasi na watu wengi.
8 Atawaua binti zako katika shamba. Ataweka kazi ya boma na kujenga ulaghai dhidi ya kuta zako na kuziinua ngao dhidi yao.
9 Ataweka vyombo vya kubomolea dhidi ya kuta zako, na vyombo vyake vitaanguka chini ya minara yako.
10 Farasi zake zitakuwa nyingi kwamba mavumbi yao yatawafunika. Kuta zako zitatikisika kwa mlio wa waendesha farasi, magurudumu, na magari ya farasi. Wakati atakapoingia malango yako, ataingia kama watu waingiavyo kwenye mji ambao kuta zimebomolewa.
11 Kwato za farasi zake zitaikanyaga mitaa yako yote. Atawaua watu wako kwa upanga na nguzo za uweza wako zitaanguka chini.
12 Watauteka nyara utajiri wako na bidhaa iliyoporwa. Watabomoa kuta zako na kuziharibu nyumba zako za kifahari. Mawe yako, mbao zako, na kokoto watazitupa kwenye maji.
13 Nitaikomesha sauti ya nyimbo zako. Sauti ya vinubi haitasikika tena.
14 Nitakufanya jiwe tupu, utakuwa mahali ambapo nyavu zitasambazwa kuzikausha. Hutajengwa tena, kwa kuwa mimi, Bwana Yahwe nimesema-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
15 Bwana Yahwe amwambia hivi Tiro, 'Je visiwa havitatetemeka kwa mlio wa kuanguka kwako, na pamoja na watakaogumia kwa jeraha wakati machinjio mabaya yatakapokuwa kati yako?
16 Kisha wakuu wote wa bahari watakaposhuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuvua mavazi yao rasmi na kutupa mavazi yaliyonakshiwa. Watavaa wenyewe kwa kutetemeka, wataketi chini na kutetemeka kila wakati, na wataogopa kwa sababu yako.
17 Watainua maombolezo juu yako na kukwambia, umekuwaje, uliyekuwa umekaliwa na manahodha wa meli, umeharibika. Mji mashuhuri ulikuwa imara sana-sasa umetoka kwenye bahari. Wale wanaoishi ndani yake wanaotia hofu kuhusu wenyewe juu ya kila mmoja aliyeishi karibu nao.
18 Sasa fukwe zitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako. Visiwa katika bahari vimeogofya, kwa sababu umekufa.'
19 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: wakati nitakapokufanya wewe mji kuwa ukiwa, kama miji mingine ambayo haikaliwi, wakati nitakapoviinua vilindi dhidi yako, na wakati maji makuu yatakapokufunika,
20 kisha nitakushusha chini kwenda kwa watu wa nyakati za zamani, kama wengingine walioenda chini kwenye shimo; kwa kuwa nitakufanya uishi katika falme za chini za dunia kama uharibifu wa nyakati za zamani. Kwa sababu hii hutarudi na kusimama katika nchi ya walio hai.
21 Nitaweka janga juu yako, na hutakuwepo tena milele. Kisha utatafutwa, lakini hutapatikana milele tena-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”