34
1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya wachungaji wa Israeli. Toa unabii na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi kwa wachungaji: Ole kwa wachungaji wa Israeli wanaojilisha wenyewe. Je! wachungaji hawapaswi kulilinda kundi?
3 Mnakula mafungu yaliyonona na mnavaa sufu. Mnawachinja walionona. Hamkuwalisha siku zote.
4 Hamkuwatia nguvu wagonjwa, wala hamkuwaponya wenye maradhi. Hamkuwafungua wale waliovunjika, hamkuwarudisha waliofukuzwa au kuwatafuta waliopotea. Badala yake, mmetawala juu yao kwa nguvu na vurugu.
5 Kisha walikuwa wametawanyika bila mchungaji, na wakawa chakula kwa wanyama wote waishio katika mashamba, walipokuwa wametawanyika.
6 Kundi langu limetawanyika juu ya milima yote na juu ya kilima kirefu, na limetawanyika juu ya uso wote wa dunia. Wala hakuna anayewatafua.
7 Kwa hiyo, wachungaji, sikilizeni neno la Yahwe:
8 Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwa sababu kundi langu limekuwa mateka na chakula kwa ajili ya wanyama katika mashamba, kwa sababu hapakuwa na mchungaji yeyote, lakini wachungaji walijilisha wenyewe na hawakulisha kundi langu.
9 Kwa hiyo, wachungaji, lisikilizeni neno la Yahwe:
10 Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu ya wachungaji, na nitalitaka kundi langu kutoka mkononi mwake. Kisha nitawaachisha kutoka kulichunga kundi; wala wachungaji hawatajilisha wenyewe tena kwa kuwa nitaliondoa kundi langu kutoka midomoni mwao, ili kwamba kundi langu lisiwe chakula kwa ajili yao tena.
11 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! mimi mwenyewe nitawatafuta kondoo wangu na kuwaulizia,
12 kama mchungaji atafutaye kundi lake juu ya siku hiyo yupo ndani ya kundi lake lililotawanyika. Hivyo nitalitafuta kundi langu, na nitalichunga kutoka sehemu lilipokuwa limetawanyika siku ya mawingu na giza.
13 Kisha nitalileta kutoka miongoni mwa watu; nitalikusanya kutoka nchi mbali mbali na kulileta kwenye nchi yao. Nitaliweka kwenye malisho juu ya pande za milima ya Israeli, karibu na vijito, na katika kila makazi katika nchi.
14 Nitawaweka kwenye malisho mema; juu ya milima ya Israeli itakuwa sehemu za malisho yao. Watalala chini huko katika sehemu nzuri kwa ajili ya malisho, katika malisho mengi, na watalisha juu ya milima ya Israeli.
15 Mimi mwenyewe nitachunga kondoo wangu, na mimi mwenyewe nitawalaza chini-hivi ndivyo Bwana Yahwe
16 asemavyo-Nitawatafuta waliopotea nitawarudisha waliofukuzwa. Nitawafunga waliovunjika na kuwaponya kondoo waliougua lakini wanene na wenye nguvu nitawaharibu. Nitawalisha kwa haki.
17 Hivyo sasa ninyi, kundi langu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-tazama, nitakuwa hakimu kati ya kondoo na kondoo na kati ya kondoo dume na mbuzi dume.
18 Je! haitoshi kulisha juu ya malisho mazuri, ambayo mtayakanyaga chini kwa miguu yenu kile kilichobakia kwenye malisho; na kunywa kutoka maji masafi, ambayo hakuna budi kuikanyaga mito kwa miguu yenu?
19 Kondoo zangu zitakula kile mlichokanyagwa kwa miguu yenu, na kunywa maji yale mliyoyakanyaga kwa miguu yenu?
20 Kwa hiyo Bwana Yahwe anawaambia hivi; Tazama! Mimi mwenyewe nitahukumu kati ya wanene na waliokonda,
21 Kwa kuwa mmewasukuma kwa ubavu wenu na mabega, na kuwapiga kwa pembe wadhaifu wote kwa pembe zenu hadi mtakapowatawanya mbali kutoka kwenye nchi.
22 Nitaliokoa kundi langu na hawatakuwa mateka tena, na nitahukumu kati ya kondoo mmoja na mwingine!
23 Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi. Atawachunga, atawalisha, na atakuwa mchungaji wao.
24 Kwa kuwa mimi, Yahwe, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu kati yao-mimi, Yahwe, nimesema hivi.
25 Kisha nitafanya agano la amani pamoja nao na kuwaondoa wanyama waovu kutoka kwenye nchi, ili kwamba waishi salama katika jangwa na walale salama katika misitu.
26 Pia nitaleta baraka juu yao na juu ya maeneo yazungukao kilima changu, kwa kuwa nitaleta manyunyu kwa wakati wake. Haya yatakuwa manyunyu ya baraka.
27 Kisha miti ya shambani itazaa matunda yake, na dunia itashindwa kuzaa matunda yake. Kondoo wangu watakuwa salama katika nchi yao; kisha watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakazipovunja fito za kongwa zao, na wakati nitakapowalinda kutoka kwenye mkono wa wale walio watumikisha.
28 Hawatakuwa mateka tena kwa mataifa, na wanyama pori juu ya dunia hawatawameza tena. Kwa kuwa wataishi salama na wala hakuna mtu atakayewatia hofu.
29 Kwa kuwa nitatengeneza sehemu ya kulimia nzuri kwa ajili yao hivyo hawataangamia kwa njaa katika nchi, na mataifa hayataleta matukano juu ya yao.
30 Kisha watajua kwamba mimi, Yahwe Mungu wao, niko pamoja nao. Ni watu wangu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.
31 Kwa kuwa ninyi ni kondoo wangu, kundi la malisho yangu, na watu wangu, na mimi ni Mungu wenu-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.”