5
1 Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao.
2 Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
3 Zinaa au uchafu wowote na tamaa mbaya lazima visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,
4 wala machukizo yasitajwe, mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.
5 Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo nimwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6 Mtu yote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
7 Hivyo usishiriki pamoja nao.
8 Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.
9 Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.
10 Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana.
11 Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.
12 Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.
13 Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,
14 kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, “Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako.”
15 Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
16 Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.
17 Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.
18 Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.
19 Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.
20 Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.
21 Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.
22 Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana.
23 Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo.
25 Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.
26 Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.
27 Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.
28 Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.
29 Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.
30 Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake.
31 “Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”.
32 huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.
33 Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.