10
1 Kisha Mfalme Ahusiero akaweka kodi juu ya nchi na maeneo ya bahari.
2 Mafanikio yote na nguvu na ukuu wake, pamoja na wa Modekai ambao mfalme alimwinua, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu ya wafalme wa Wamedi na Waajemi.
3 Modekai Muyahudi alikuwa wa pili kutoka kwa Mfalme Ahusiero. Alikuwa mkuu na maarufu miongoni mwa ndugu zake Wayahudi, kwa sababu alitetea mahitaji ya watu wake na haki za watu na akatetea amani kwa watu wote.