3
1 Baada ya mambo haya, Mfalme Ahusiero alimpandisha cheo Hamani mwana wa Hammedatha mwagagi, na akaweka kiti chake cha ukuu juu ya wakuu wote waliokuwa pamoja naye.
2 Na watumishi wote wa mfalme waliokuwa katika lango la mfalme walipaswa kupiga magoti na kusujudia Hamani, kama mfalme alivyoagiza. Lakini Modekai hakupiga magoti wala kusujudu mbele ya Hamani.
3 Kisha watumishi wa mfalme waliokuwa langoni mwa mfalme walimwambia Modekai, kwa nini hautii amri ya mfalme?
4 Walisema naye siku kwa siku, lakini alikataa kufuata matakwa yao. Hivyo wakaongea na Hamani kuona kama swala la Modekai lingebaki hivyo alikuwa amewataarifu kuwa Modekai alikuwa Muyahudi.
5 Hamani alipoona kuwa Modekai hapigi magoti wala kumsujudia, alipatwa na hasira.
6 Alikuwa na wazo la kumuua Modekai, watumishi wa mfalme walikuwa wamemueleza kuwa Modekai na jamaa zake walikuwa Wayahudi. Hamani akaazimu kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wa Modekai, ambao walikuwa katika ufalme wa Ahusiero.
7 Katika mwezi wa kwanza, (ambao ni mwezi wa Nisani) ndani ya mwaka wa kumi na mbili wa Mfalme Ahusiero, walipiga kura mbele ya Hamani kura kila siku na mwezi, kuchagua siku na mwezi hadi walipochagua mwezi wa kumi na mbili, (mwezi wa Adari.
8 Kisha Hamani akamwambia mfalme Ahusiro, “kuna watu fulani katika majimbo yote ya ufalme wako wasiofuata sheria zako. Na kwa tabia yao ya kutofuata sheria zako hawapasi kuendelea kuwa hai.
9 Kama ikimpendeza mfalme, toa amri watu hawa wote wakatiliwe mbali, nami nitapima talanta elfu kumi za fedha katika mikono ya wale ambao ni wasimamizi wa maswala ya mfalme, ili kwamba waweke katika hazina ya mfalme.”
10 Ndipo mfamle akavua pete yake ya muhuri na kumpa Hamani, adui wa Wayahudi.
11 Mfalme akamwambia Hamani, “Nitahakikisha kwamba fedha inarudi kwako na kwa watu wako. Ili muitumie kama mpendavyo.”
12 Kisha waandishi wa mfalme walikusanyika katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, na mbiu iliyokuwa na matakwa ya Hamani yalikuwa yameandikwa na kupelekwa kwa wasimamizi wa majimbo, na wale wote waliokuwa juu ya wasimamizi wa majimbo yote, na wasimamizi wa watu, na kwa kila jimbo kwa andiko lao, na kila watu na lugha yao. Mbiu hii ilikuwa imeandikwa kwa jina la mfalme Ahusiero na kupigwa muhuri wa pete yake.
13 Barua hizi za kutaka kuwakatilia mbali Wayahudi wote zilizambazwa katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kuangamiza, kuua na kuwaharibu Wayahudi wote, tangu mdogo hadi mkubwa, watoto na wanawake, ndani ya siku moja katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili (ambao ni mwezi wa Adari) na kuteka mali zo.
14 Nakala ya ilifanywa kuwa sheria na kupelekwa kila jimbo. Taarifa juu ya maangamizi ya Wayahudi ilienea katika kila jimbo kwamba watu wote wajiandae katika siku hiyo.
15 Wasambazajia walisambaza agizo la mfalme. Tangazo hili pioa lilitolewa na kusambazwa katika mji wa Shushani. Mfalme alikuwa na Hamani walikaa na kunywa, lakini mji wa Shushani, lakini mjiwa Shushani ulikuwa katika uangamivu.