11
1 Miti itachipukia katika mizizi ya Yese, na matawi yanayotokana na mizizi yatazaa matunda.
2 Na roho wa Bwana atashuka juu yake, roho wa hekima na maelewano, roho ya maelekezo na ukuu, roho ya maarifa na hofu ya Yahwe.
3 Furaha yake itakuwa hofu ya Bwana; hatatoa hukumu kwa kile anachokiona, wala atatoa maamuzi kwa kile anachokisikia.
4 Badala yake atawahukumu masikini kwa haki na atafanya maamuzi kwa usawa na unyenyekevu. Ataamurisha mgomo wa dunia kwa fimbo ya mdomo wake, na punzi ya midomo yake, atawauwa waovu.
5 Haki itakuwa mkanda wa viuno kiuno chake kuzunguka mapaja yake.
6 Mbwa mwitu atakaa pamoja na kondoo, na chui watalala chini pamoja na mtoto wa mbuzi, ndama, mtoto wa simba na ndama pamoja na ndama aliyenona. Mtoto mdogo atawaongoza wao.
7 Ng'ombe na dubu watachungwa pamoja. Na watoto wao watalala pamoja. Simba atakula majani kama ng'ombe.
8 Mtoto atacheza juu ya chimo la nyoka, na mtoto aliyeachwa ataweka mkono wake katika pango la nyoka.
9 Hawataumizwa wala kuharibiwa kwenye mlima mtakatifu; kwa maana dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe, kama maji yajaavyo kwenye bahari.
10 Siku hiyo mzizi wa Yese utasimama kama bendera ya watu. Taifa litamtafuta yeye nje, na mahali pake pakupumzikia patatukuka.
11 Siku hiyo, Bwana ataunyoosha mkono wake tena kuokoa mabaki ya watu wake yaliyosalia huko Asiria, Misri, Pathrosi, Kushi, Shinari, Hamathi, na kisiwa cha bahari.
12 Ataweka bendera kwa kwa mataifa na atakusanya Waisrel waliotupwa na watu wa Juuda waliotawanyika kitika pembe nne za dunia.
13 Ataujeuza wivu wa Efraimu, na ukatili wa Yuda utakomeshwa. Efraimu atamuonea wivu Yuda, Yuda hatakuwa adui wa Efraimu tena.
14 Badala yake, watashuka chini kwenye mlima wa Wafilisti upande wa magharibi, na pamoja watateka watu mashariki. Watavamia Edomu na Moabu, na watu wa Amoni watawatii wao.
15 Yahwe atauharibu kabisa ghuba ya bahari ya Misri. Kwa mawimbi makali ambayo yanavuma juu ya mtoto Efurate na itagawanyika katika mifereji saba, hivyo unaweza ukapita juu kwa viatu.
16 Kutakuwa na njia kuu kwa ajili ya mabaki ya watu kurudi kutoka Asiria, maana kuna Waisraeli wanaokuja kutoka nchi ya Misri.