20
1 Katika mwaka ambao Tartani alipofika kwa Ashdodi, alipotumwa na Sarjoni mfalme wa Asiria, nae akapigana na Ashdodd na akachukua.
2 Mda huo Yahwe alizungumza na Isaya mwana wa Amozi, ''Nenda ukaondoe nguo za magunia katika kiuno chako, na ondoeni viatu vyenu kwenye miguu.'' Alifanya hivyo, tembeeni uchi na miguu wazi.
3 Yahwe asema, ''Kama ilivyokuwa kwa mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na pasipo kuvaa viatu kwa miaka mitatu, ni ishara na dalili kuhusu Misri na kuhusu Ethiopia—
4 katika njia hii mfalme wa Asiria atawaongoza mateka wa Misri, na walioko uhamishoni Ethiopia, watoto kwa wazee, waliouchi na wasio na viatu, na ambao hawajajisitiri kuiweka Misri katika aibu.
5 Watafadhaika na kuona aibu, kwa sababu ya Ethiopia ni matumaini yao na Misri ni utukufu wao.
6 Wenyeji wa pwani hiiwatasema siku hiyo, 'Kweli, hichi ndicho chanzo chetu cha matumaini, tulipokimbilia kuhitaji msaada kutoka kwa mfalme wa Asiria, je ni kwa jisi gani tunaweza kupona?''