22
1 Tamko kuhusu bonde la maono:
2 Mji wenye kelele, mji umejaa maovu; wafu hawajauwawa kwa upanga, na hawakuuwawa kwenye vita.
3 Viongozi wenu wamekimbia pamoja, lakini wamekamatwa pasipo na upinde, wote kwa pamoja wamekamatwa na wamekamatwa pamoja; walikimbia kutoka mbali.
4 Hivyo basi, Msiniangalie mimi, nitalia kwa uchungu; msijaribu kunifariji kuhusiana na kuharibika kwa binti ya watu wangu.
5 Maana kuna siku za ghasia, akanyagaye chini, na fujo za Bwana, Yahwe wa majeshi, katika bonge la maono, kuanguka chini kwa ukuta, na watu wanalia juu ya milima.
6 Elamu chukua podo juu, na gari la watu na farasi, na kirghizameweka ngao wazi.
7 Siku hiyo ambapo mabonde ulioyachagua yatajaa magari, na farasi watachukua nafasi zao katika lango.
8 Atauodoa mbali ulinzi wa Yuda; na utaona siku hiyo utaona silaha katika jumba la msitu.
9 Umeona matawi ya mji wa Daudi, jinsi mlivyowengi, na kukusanya maji katika birika la chini.
10 Umehesabu nyumba za Yerusalemu, na umerarua nyumba chini kuuimarish ukuta.
11 Na umefanya hifadhi katika ya kuta mbili maana maji ya birika la zamani. Maana haukuwahusisha walioujenga mji, walioupanga mji kutoka zamani.
12 Bwana, Yahwe wa majeshi amewaita siku hiyo watu waje kuomboleza na kulia, wanyoe vichwa vyao na kuvaa nguo za magunia.
13 Lakini angalia, badala yake sherehe na furaha, kuuwa ng'ombe na kuchinga kondoo, njooni tule na kunjwa mvinjo maana kesho tutakufa.
14 Hili limebanika kwenye masikio yangu na Yahwe wa majeshi: Hakika maovu haya hayatasamehewa, hata utakapokufa, ''Amesema Bwana wa majeshi.
15 Bwana, Yahwe wa majeshi, asema hivi, ''Nenda kwa huyu kiongozi, kwa Shebana, aliye juu ya nyumba, na umwambie,
16 Ni nina aliyekuruhusu kuchimba kaburi lako mwenyewe, kukata juu ya kaburi na juu ya urefu katika mahali pa kupunzikia ndani mwamba?''
17 Yahwe anakaribia kukutupa chini; mtu mwenye nguvu, anakaribia kukutupa chini; atakuzongazonga.
18 Atahakikisha anatuzungusha zungusha, na kutupa msukosuko kama mpira kwenye nchi kubwa. Pale utakapokufa, na pale gari lako tukufu litakapo kuwa; utakuwa aibu ya nyumba ya bwana wako!
19 ''Nami nitakuondoa katika ofisi yako na katika kituo chako. Na utavutwa chini.
20 Na itakuwa hivi kuhusu siku hiyo nitamchukua Eliakimu mtoto wa Hilkia mtumishi wangu.
21 Nitamvisha yeye kwa kanzu yenu na kumvika mkanda wenu, na nitahamisha mamlaka yenu kwenye mikono yake. Atakuwa baba wa wenyeji wa Yerusalemu na katika nyumba ya Yuda.
22 Nitaziweka funguo za nyumba ya Daudi kwenye mabega yake; Atafungua, na hakuna atakayefunga; na atafunga na hakuna atakayefungua.
23 Nami nitamuimarisha yeye, kigingi katika mahali salama, na atakuwa kiti cha utukufu katika nyumba ya baba yake.
24 Nao wataangukia juu yake utukufu wote wa baba nyumba ya baba yake, watoto wake na uzao wake na kila chombo kidogo kutoka vikombe mpaka majagi yote.
25 Siku hiyo- hili ndilo tamko la Yahwe wa majeshi- kigingi kilichowekwa katika mazingira imara kitatoa njia, utavunjika, na kuanguka, na uzito ulionao utaondoleawa- maana Yahwe amesema.