34
1 Njooni karibu enyi mataifa, sikilizeni na muwe makini, enyi watu! Dunia na vyote vijazavyo vinatakiwa kusikiliza, dunia na vyote vitokavyo,
2 Maana Yahwe ana hasira na mataifa yote, ana hasira dhidi ya majeshi yao; amewaangamiza wao kabisa, ameawakabidhi kwa wachinjaji.
3 Miili ya watu wao waliokufa itatupwa nje. Harufu ya miili iliyokffa itakuwa kila mahali; na mlilima italowekwa kwa damu yao.
4 Nyota zote angani zitafifia, na anga litakunjwa kama kitabu; na nyota zake zitafifia mbali, kama tawi linavyonyauka kwenye mzabibu, kama tunda lilokomaa kwenye mti.
5 Maana pale upanga wangu utakapokunywa na kushiba mbinguni; tazama, maana sasa utakuja chini huko Edomu, kwa watu ambao nimewaweka mbali na adhabu.
6 Upanga wa Yahwe unadondosha matone ya damu na kufunikwa kwa mafuta, matone ya damu ya kondoo na mbuzi, yamefunikwa kwa figo za kondoo. Maana Yahwe ametoa sadaka katika Bozra na mauwaji katika nchi ya Edomu.
7 Ng'ombe wa porini watachinjwa pamoja na wao, fahali wakubwa na fahali wadogo. Nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatafanjwa kuwa mafuta na mafuta yaliyonona.
8 Maana itakuwa ni siku ya kisasi kwa Yahwe na mwaka ambao anawalipa kwa sababu ya Sayuni.
9 Mifereji ya Edomu itageuka kuwa lami, na mavumbi yake yatakuwa kiberiti na nchi itakuwa kama lami inayoungua.
10 Itaungua usiku na mchana; moshi wake utatoka daima; na patakuwa nyika kizazi hata kizazi; na hakuna hata mmoja atakayepita hapo milele na milele.
11 Lakini ndege na wanyama porini wataishi pale; bundi na kunguru watatengeneza viota vyao pale. Atanjoosha juu yake futi kamba ya uharibifu na pima maji ya uharibifu.
12 Wenye vyeo hawatakuwa na kitu kilichobakia kuita ufalme, na wakuu wote watakuwa si kitu.
13 Miiba itaota katika maeneo yao, viwavi na mbigiri vitakuwa katika ngome zao. Yatakuwa makao ya mbweha, makazi ya mbuni.
14 Wanyama wa porini na fisi watakusanyika pale, na mbuzi wa porini watalia wao kwa wao. Nyakati za usiku wanyama watakaa pale na watajitafutia wenywe mahali pa kupumzikia.
15 Bundi watatengeneza viota vyao, na kutotolea mayai yao, kila mmoja na mwenzake.
16 Kutafuta kupitia kitabu cha Yahwe; hakuna hata kimoja ambacho hakitakuwepo. Hakuna kitakacho kosa mwenzake; maana mdoma wake umeamuru hivyo, roho yake imewakusanya wao.
17 Atapiga kura katika eneo lao, na mkono wake umewapima kwa kamba. Wataimiliki daima; kutoka kizazi hata kizazi wataishi pale.