4
1 Siku hiyo wanawake saba watamchukua mwanaume mmoja na kusema, ''Tutakula chakula chetu wenyewe, tutavaa nguo zetu wenyewe. lakini tunahitaji kuchukua jina lako ili tuondoe haibu zetu.''
2 Na siku hiyo tawi zuri la Yahwe na utukufu, na matunda yatakuwa na ladha nzuri na kupendeza kwa wale wanaoishi Israeli.
3 Itatokea kwa yule aliyeachwa Sayuni na wale waliobakia Yerusalemu wataitwa watakatifu, yeyeto aliyeandikwa chini anaishi Yerusalemu.
4 Hii itatokea pale ambapo Bwana atasafisha uchafu wa mabinti wa Sayuni, na atasafisha madoa ya damu kutoka kati ya Yerusalemu, kwa namna ya roho ya hukumu na roho ya kuungua na moto.
5 Tena juu ya mlima wote wa Sayuni na mahali pakuksanyikia, Yahwe atafanya wingu na moshi kwa wakati wa mchana na moto unaong'a wakati wa usiku; na itakuwa dari juu ya utukufu wote.
6 kutakuwa na kivuli kwenye makazi wakati mchana kuzuia jua, na kimbilio na mfuniko kutoka kwenye mawimbi na mvua.