42
1 Tazama, mtumishi wangu, niliyekushika; niliyekuchagua, kwake ninapata furaha. Nimeiweka roho yangu juu yake; ataleta haki kwa mataifa.
2 Hatalia wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika mitaani.
3 Mwanzi ulioangamizwa hatauvunja, na wala utambi unaowaka na kutoa mwanga hautaungua: atatekeleza haki kwa uaminifu.
4 wala hatazimia wala kukata tamaa mpaka atakapoanzisha haki katika nchi; na pwani inasubiria sheria yake.
5 Mungu Yahwe asema hivi—yeye aliyeziumba mbingu na yeye zinyoosha nje, yeye aliyeiumba nchi na vitu vyote izalishavyo, yeye aliyewapa punzi watu na wale waishio juu:
6 Mimi Yahwe nimekuita kwa haki yangu na nitakushika kwa mkono wangu. Nitakutunza wewe, na nitakuweka wewe kama agano kwa watu wangu, kama mwanga wa wayunani
7 Kuyafungua macho ya vipofu, kuwatoa waliofungwa gerezani, kuwatoa wale walio gizani kutoka kwenye nyumba iliyofungiwa.
8 Mimi ni Yahwe, Hilo ndilo jina langu; na utukufu wangu sitashiriana na mtu mwingine wala sifa zangu sitashirkiana na sanamu ya kuchonga.
9 Tazama, mambo ya nyuma yamekuja na kupita, sasa ninakaribia kutangaza mambo mapya. Kabla hayajaanza kutokea nitawambia kuhusu wao.''
10 Mwimbieni Yahwe wimbo mpya, na sifa zake kutoka mwisho wa nchi; wewe ushukae chini kwenye bahari, na vyote vilivyomo ndani yake, waishio pwani na wale wanaoishi huko.
11 Wacha jangwa na miji ilie, vijiji anavyoishi na Kaderi, lia kwa furaha! waache wenyeji wa Sela waimbe; waache wapige kelele juu ya kilele cha mlima.
12 waache wamtukuze Yahwe na kutangaza sifa zake katika aridhi ya pwani.
13 Yahwe atatoka nje kama shujaa; kama mtu wa vita ataichochea bidii yake. Atapiga kelele, ndio, atalia kw kishindo katika vita yake; atawaonyesha adui zake nguvu zake.
14 Nimenyamaza kimyi kwa mda mrefu; bado nimendelea kujizuia mimi mwenyewe; Nitalia kama mwanamke anayetaka kuzaa; nitatweta na kuugua.
15 Nitaiharibu milima na vilima na kukausha uoto wake wa asili; nitajeuza mito kuwa visiwa na nitakausha matindiga.
16 Nitawaleta vipofu kwa njia wasioijua; katika njia wasiyoijua Nitawapitisha wao. Nitaligeuza giza kuwa mwanga mbele yao, na kupanyoosha mahali palipopotoka. Mambo yote haya nitayafanya, na sitaachana na wao.
17 Watageuka nyuma, wataabishwa sana, wale wote wanaoiamini sanamu ya kuchonga, wanaosema na kuziambia sanamu za chuma, ''Nyinyi ni miungu wetu.''
18 Sikilizeni ewe kiziwi; tazama, ewe kipofu, ili uweze kuona.
19 aliye kipofu ila mtumishi wangu? au kiziwi ni kama mjumbe niliyemtuma? Ni nani aliye kipofu kama mpenzi wangu wa agano, au kipofu kama mtumishi wa Yahwe?
20 Mmeona mambo mengi, lakini hamuelewi; masikio yamefunguka, lakini hakuna anayesikia.
21 Itampendeza Yahwe kuisifu haki yake na kuitukuza sheria yake.
22 Lakini watu hawa ni wale waliokamtw na kutekwa; wote wamenaswa kwenye mashimo; wafungwa wote wamewekwa gerezani; wamekuwa mateka na hakuna hata mmoja wa kuwaokoa wao, hakuna asemaye, warudisheni.''
23 Ni nani miongoni mwenu atalisikiliza hili? nani atayasikia na ni nani atasikia wakati ujao?
24 Ni nani aliyemtoa Yakobo kwa majambazi, na Israeli kwa wanyang'anyi? Je hakuwa Yahwe, dhidi ya wale waliotenda dhambi, waliokataa kutembea katika njia zako na wale waliokataa kusheshimu sheria yako.
25 Hivyo basi humwaga asira yake kali nje dhidi yao, kwa uharibifu wa vita. Iliwaka kuwazunguka wao, hata hawakujua hilo, lakini hawakuyachukulia hayo moyoni mwao.