58
1 ''Lia kwa sauti; usinyamaze. Paza sauti yako juu kama mbiu. Kabiliana na watu wangu wenye uasi, na nyumba ya Yakobo na dhambi zao.
2 Bali wananitafuta mimi kila siku na kufurahia katika maarifa ya njia zangu, kama taifa linalotenda haki na hawakuiacha sheria ya Mungu wao. Wananiuliza mimi kuhusu hukumu ya haki; wamepata furaha katika mawazo yao ya kwa kumkaribia Mungu
3 Kwa niini tulifunga; walisema, 'Lakini hamkuona hilo? Kwa nini tulijinyenyekeza wenywe, lakini hakutambua?' Tazama, siku ya kufunda kwanu utatafuta furaha yanu mwenyewe na kuwanyanyasa wafanyakazi wenu wote.
4 Tazama, ninyi mnafunga ili muwe wepesi wa kugombana na kupigana, na kupiga kwa ngumi ya uovu wako; haujafunga leo kuifanya sauti yako isikike juu.
5 Kwa uhalisi aina ya mfungo huu ndio ambao ninauhitaji: Siku ambayo kila mtu hunyenyekea mwenyewe, huinamisha kichwa chake chini kama mwanzi, na hutawanya mavazi ya magunia na majivu chini yake? Je kweli unauita huu ni mfungo, siku ya kumfurahisha Yahwe.?
6 Hii sio mfungo ambao niliuchagua mimi: kufungua vifungo vya waovu, kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioangamizwa, na kuharibu kila nira?
7 Sio kwamba kula mkate na wenye njaa na kuwaleta masikini na kuwaleta wasio na makazi katika nyuma yako?'' Unapomuana mtu yuko uchi, unatakiwa vumvishe mavazi; na usijifiche mwenyewe na ndugu zako.
8 Halafu mwanga wako utafunguliwa kama jua, na uponyaji wako utachipukia juu kwa haraka; haki yako itaenda mbele zake, na na utukufu wa Yahwe utakuwa nyuma kukulinda.
9 Halafu utamuita, na Yahwe atakuitikia; utalia ukihitaji msaada, na atasema, ''Nipo hapa.'' Ikiwa utaitoa nira isiwepo miongoni mwako, kidole kinachoshataki, maongezi ya waovu,
10 Ikiwa wewe mwenyewe utawapa wenye njaa na kuwaridhisha wahitaji katika shida, na giza lako litakuwa kama mchana.
11 Halafu Yahwe ataendelea kuwaongoza ninyi na kuwa ridhisha ninyi katika mikoa ambayo hakuna maji, Ataimarisha mifupa yenu. Mtakuwa kama bustani iliyonyeshewa maji, na kama mkondo wa maji, ambaopo maji yake hayapungui.
12 Baadhi yenu mtajenga tena sehumu za kale zilizoharibiwa; mtatengeneza sehemu zilizoharibiwana vizazi vingi; na mtaitwa ''Mrekebishaji wa ukuta,'' kuwarejesha katika mtaa ya kuishi.''
13 Tuseme kwamba ukigeuza nyuma miguu yenu kutoka safarini katika siku ya sabato, kufanya anasa siku yangu takatifu, Tuseme kwamba umeiita sabato siku ya furaha, na umeiita siku ya Bwana Yahwe mtakatifu na yenye kuheshimiwa. Tuseme kwamba unahieshimu sabato kwa kuacha biashara zako, na hautafuti anasa zako mwenyewe na uzungumzi maneno yako mwenyewe.
14 ''Halafu utapata furaha kwa Yahwe; na nitaifanya safari yako juu ya urefu wa nchi; Nitakulisha wewe kwenye urithi wa Yakobo baba yenu- maana mdomo wa Yahwe umezungumza.''