22
Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema, Je mtu anaweza kumfaa Mungu “Je mwenye hekima anaweza kufaa kwake. Je inafurahisha kwa Mwenyezi ikiwa u mwenye haki? Je ni faida yake ukiyafanya safi maisha yako? Je ni kwa sababu ya uchaji wako kwake hata akukemee na kukuadhibu? Je si kwa sababu ya wingi wa uovu wako? Je hakuna mwisho wa makosa yako? Kwa maana umechukua dhamana kutoka kwa ndugu yako bila sababu; umechukua mavazi ya mtu na kumwacha uchi. Haukuwapa wenye kiu maji ya kunywea; umewanyima chakula wenye njaa japokuwa wewe, mwenye uwezo, uliimiliki nchi, japokuwa wewe, mwenye kuheshimiwa, uliishi ndani yake. Umewaacha wajane waondoke bila kitu; umewatesa yatima. 10 Kwa hiyo, mabaya yanakuzunguka, na hofu za ghafla zinakusumbua. 11 Kuna giza, hata usione; gharika inakufunika. 12 Je Mungu hayupo juu mbinguni? Anaangalia juu ya nyota, jinsi zilivyo juu! 13 Unasema, 'Mungu anajua nini? Je anaweza kuamua kupitia giza totoro? 14 Mawingu ni kifuniko chake, hata asituone; anatembea anga la mbinguni.' 15 Je utayaishi maisha ya zamani walioishi waovu - 16 walioondolewa kabla ya siku zao, ambao misingi yao imeondolewa kama mto, 17 waliomwambia Mungu, 'Ondoka kwetu'; waliosema, 'Mwenyezi anaweza kututenda nini? 18 Hata hivyo bado alizijaza nyumba zao kwa mema; mipango ya waovu iko mbali nami. 19 Wenye haki wanayaona yawapatayo waovu na kufurahi; wasio na hatia wanawacheka kwa dhihaka. 20 Wanasema, 'Bila shaka walioinuka kinyume chetu wameondolewa; moto umeteketeza mali zao.' 21 Basi patana na Mungu na uwe na amani naye; kwa njia hiyo, mema yatakujia. 22 Nakusihi, pokea, maelekezo yake; uyatii maneno yake. 23 Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa, ukiacha kutenda uovu makaoni mwako. 24 Weka hazina zako mavumbini, dhahabu ya Ofiri kati ya mawe ya vijito, 25 na Mwenyezi atakuwa hazina zako, fedha ya thamani kwako. 26 Nawe utajifurahisha katika Mwenyezi; utamwangalia Mungu. 27 Utamwomba, naye atakusikiliza; utamtolea nadhiri. 28 Lakini pia utatamka lolote, nawe utapewa; nuru itaangaza maishani mwako. 29 Mungu humshusha mwenye kiburi, naye humwinua mnyenyekevu. 30 Atamwokoa asiye na hatia; utaokolewa kupitia usafi wa mikono yako.”