Yona
1
1 Ndipo neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amittai, kusema,
2 “Simama uende Ninawi, mji kuu, na ukapaze sauti dhidi yake, kwa sababu uovu wao umeinuka mbele yangu.”
3 Lakini Yona akaondoka kukimbia kutoka mbele ya Bwana na kwenda Tarshishi. Akatelemka mpaka Yafa na akaona melikebu inayokwenda Tarshishi. Kwa hiyo alilipa nauli na akapanda melikebu kwenda nayo Tarishishi, mbali na uwepo wa Yahweh.
4 Lakini Bwana akatuma upepo mkubwa juu ya bahari, ikawa tufani juu ya bahari. Hivi karibuni ikaonekana kwamba meli ilikuwa inataka kuvunjika.
5 Wale baharia waliogopa sana na kila mtu alilia kwa mungu wake mwenyewe. Wakatupa mizigo bahari iliyokuwa merikebuni ili kuifungua. Yona alikuwa ameshuka hapa pande za ndani ya melikebu, naye alikuwa amelala huko usingizi.
6 Basi nahoza akamwendea akamwambia, “kwa nini unalala? Amka! ukamwombe mungu wako! Labda mungu wako atatutambua na hatutapotea.”
7 Wote wakaambiana, 'Njoni, tupige kura, ili tujue ni nani ndiye sababu ya mabaya haya yanayotupata.' Basi wakapiga kura, na kura ikaangukia kwa Yona.
8 Kisha wakamwambia Yona, “Tafadhali tuambie ni nani ndiye sababu ya mabaya haya yanayotupata. Unafanya kazi gani, na umetoka wapi? Nchi yako ni ipi, na kutoka kwa watu wa kabila gani?”
9 Yona akawaambia, Mimi ni Mhebrania; Nami namuogopa Bwana, Mungu wa mbinguni, aliyeifanya bahari na nchi kavu.
10 Ndipo watu hao waliogopa zaidi, wakamwambia Yona, Ni jambo gani hili ulilolifanya? Kwa maana hao watu walijua kwamba alikuwa akikimbia mbele ya Bwana, kwa sababu alikuwa amewaambia.
11 Ndipo wakamwambia Yona, Tukufanyie nini ili bahari iweze kutulia? Kwa maana bahari ilikuwa imechafuka zaidi na zaidi.
12 Yona akawaambia, “Nikamateni na nitupeni baharini. Kisha bahari itatulia kwa ajili yenu, kwa maana najua kwamba ni kwa sababu yangu kwamba tufani hii kubwa iwapate.”
13 Hata hivyo, watu hao wavuta makasia kwa bidii ili kurudi nchi kavu, lakini hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu bahari ilikuwa imechafuka zaidi dhidi yao.
14 Basi wakamwomba Bwana, wakasema, Tunakuomba, Bwana, tunakuomba, usiache tuangamize kwa sababu ya maisha ya mtu huyu; wala usituwekee hatia ya kufa kwake, kwa kuwa wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.
15 Basi wakamchukua Yona wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.
16 Ndipo watu wale wakamuogopa Bwana sana. Wakamtolea dhabihu Bwana na kuweka nadhiri.
17 Bwana alikuwa ameandaa samaki mkubwa kummeza Yona, na Yona alikuwa ndani ya tumbo lasamaki siku tatu na usiku wa tatu.