10
Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi. Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje. Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake. Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.” Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao. Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo. Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza. Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho. 10 Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele. 11 Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo. 13 Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo. 14 Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi. 15 Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena. 18 Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.” 19 Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya. 20 Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?” 21 Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?” 22 Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu. 23 Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani. 24 Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi. 25 Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu. 26 Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu. 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi. 28 Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu. 29 Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba. 30 Mimi na Baba tu mmoja.” 31 Wakabeba mawe ili wamponde tena. 32 Yesu akawajibu, “Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kuniponda mawe?” 33 Wayahudi wakamjibu, “Hatukupondi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu.” 34 Yesu akawajibu, “Haikuandikwa katika sheria yenu, 'Nilisema, “Ninyi ni miungu”'?” 35 Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa), 36 mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, 'Unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'mimi ni Mwana wa Mungu'? 37 “Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini. 38 Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba.” 39 Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao. 40 Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko. 41 Watu wengi wakaja kwa Yesu. Waliendelea kusema, “Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli.” 42 Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.