19
Basi Pilato alimchukua Yesu na kumchapa. Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau. Wakamjia na kusema, “Wewe mfalme wa Wayahudi! na kisha kumpiga kwa mikono yao. Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, “Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake.” Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, “Tazameni mtu huyu hapa!” Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe, msulubishe.” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake.” Wayahudi wakamjibu Pilato, “Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu.” Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa, akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, “Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu. 10 Kisha Pilato akamwambia, “Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?” 11 Yesu akamjibu, “Usingekuwa na nguvu dhidi yangu kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo, mtu aliyenitoa kwako ana dhambi kubwa.” 12 Kutokana na jibu hili, Pilato akataka kumwacha huru, lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema, “Kama utamwacha huru basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme hunena kinyume cah kaisari.” 13 Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha. 14 Siku ya maandalizi ya pasaka ilipofika, panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni mfalme wenu huyu hapa!” 15 Wakapiga kelele, “Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!” Pilato akawaambia, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” Naye Kuhani mkuu akajibu, “Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari.” 16 Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulibiwe. 17 Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha. 18 Ndipo walipomsulibisha Yesu, pamoja naye wanaume wawili, mmoja upende huu na mwingine upande huu, na Yesu katikati yao. 19 Kisha Pilato akaandika alama na kuiwekwa juu ya msalaba. Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETH, MFALME WA WAYAHUDI. 20 Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani. 21 Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato, “Usiandike, 'Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema mimi ni mfalme wa Wayahudi.” 22 Naye Pilato akawajibu, “Niliyoandika nimeandika.” 23 Baada ya askari kumsulibisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo, Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu. 24 Kisha wakasemezana wao kwa wao, “Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani.” Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura.” 25 Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu. 26 Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!” 27 Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake. 28 Baada ya hilo, Hali Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, “Naona kiu.” 29 Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake. 30 Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake. 31 Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe. 32 Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu. 33 Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake. 34 Hata hivyo, mmoja wa askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki, na mara yakatoka maji na damu. 35 Naye aliyeona hili ametoa ushuhuda, na ushuhuda wake ni wa kweli. Yeye anajua kuwa alichokisema ni cha kweli ili nanyi pia muamini. 36 Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, “Hakuna hata wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Tena andiko lingine husema, “Watamtazama yeye waliyemchoma” 38 Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu. 39 Naye Nicodemo ambaye hapo awali alimfuata Yesu usiku naye akaja. Yeye alileta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata uzito wa ratili mia moja. 40 Kwa hiyo wakauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi wakati wa kuzika. 41 Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo. 42 Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.