43
1 Ilitokea kwamba Yeremia alimaliza kuhubiri kwa watu wote maneno yote ya Yahwe Mungu wao kwamba Yahwe Mungu wao alimwambia kusema.
2 Azaria mwana wa Hoshaia, Yonathani mwana wa Karea, na watu wenye kiburi walisema kwa Yeremia, “Unasema uongo. Yahwe Mungu wetu hajakutuma wewe kusema, 'Usiende Misri kuishi huko.'
3 Kwa kuwa Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu kututoa sisi kwenye mkono wa Wakaldayo, kwa kuwa wewe umesababisha kifo chetu na kutufanya sisi mateka huko Babeli.”
4 Basi Yonathani mwana wa Karea, wakuu wa jeshi, na watu wote walikataa kusikiliza sauti ya Yahwe kuishi kwenye nchi ya Yuda.
5 Yonathani mwana wa Karea na amri jeshi wote waliwachukua mabaki wa Yuda ambao walikuwa wamerudi kutoka mataifa yote ambapo walikuwa wametawanyika kuishi katika nchi ya Yuda.
6 Waliwachukua wanaume na wanawake, watoto na mabinti wa mfalme, na kila mtu ambaye Nebuzaradani, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliruhusu kubaki pamoja na Gedali mwana wa Ahikam mwana wa Shafan. Pia walimchukua Yeremia nabii na Baruku mwana wa Neria.
7 Walienda nchi ya Misri, kwa Tahpanhesi, kwa sababu hawakusikiliza sauti ya Yahwe.
8 Basi neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia huko Tahpanhesi na kusema,
9 “Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwenye macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi.
10 Kisha wakasema nao, “Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Ona, nimekaribia kutuma wajumbe kumchukua Nebukadreza mfalme wa Babeli kama mtumwa wangu. Nitaweka kiti cha enzi juu ya mawe haya ambayo wewe, Yeremia, umeyazika. Nebukadreza ataweka banda lake juu yao.
11 Kwa kuwa atakuja na kuvamia nchi ya Misri. Yeyote aliyeandikiwa kufa atakufa. Yeyote aliyeandikiwa mateka atachukuliwa mateka. Na yeyote aliyeandikiwa kwa upanga atakufa kwa upanga.
12 Kisha nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri. Nebukadreza atawachoma na kuwashika. Atasafisha nchi ya Misri kama wachungaji wanavyosafisha wanyama waharibio nguo zao. Ataenda nje kutoka eneo hilo kwa ushindi.
13 Atavunja nguzo za mawe huko Heliopolisi kwenye nchi ya Misri. Atachoma mahekalu ya miungu ya Misri.”