45
1 Hili ni neno ambalo Yeremia nabii alimwambia Baruku mwana wa Neria. Hii ilitokea wakati alipoandika kwenye kitabu maneno haya kwa imla ya Yeremia - hii ilikuwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, na alisema,
2 “Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi kwako, Baruku:
3 Umesema, Ole mimi, kwa kuwa Yahwe ameongeza uchungu wa maumivu. Kuugua kwangu kumenichosha; sipati pumziko.'
4 Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: “Yahwe asema hivi: Ona, nilichojenga, sasa ninararua chini. Nilichopanda, sasa ninangoa. Hii ni kweli juu ya dunia.
5 Lakini unategema mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja kwa binadamu wote - hii ni tamko la Yahwe - lakini ninakupa maisha yangu kama nyara popote utakakoenda.”