13
Sasa Yoshua alikuwa mzee wakati Yahweh alipomwambia, “Umekuwa mzee, lakini bado kuna nchi kubwa ya kuteka. Nchi iliyosalia ndio hii: mikoa yote ya Wafilisti, na mikoa ile ya Wageshuri, (tangu Shihori, iliyoko mashariki mwa Misri, na upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Ekroni, inayofikiriwa kuwa ni mali ya Wakanaani; wafalme watano wa Wafilisti, wale wafalme wa Gaza, Ashidodi, Ashikeloni, Gathi na Ekroni - miliki ya Waavi. Katika upande wa kusini, kulisalia nchi yote ya Wakanaani, na Meara ambayo ni miliki ya Wasidoni, hadi Afeki, hata mpaka wa Waamori; nchi ya Wagebali, Lebanoni kuelekea upande wa mapambazuko ya jua, kutoka Baali- Gadi chini ya Mlima Hermoni mpaka Lebo Hamathi. Pia, wenyeji wote wa nchi ya milima kutoka Lebanoni hadi Misrefothi - Maimu, pamoja na watu wa Sidoni. Nitawafukuza mbele ya jeshi la Israeli. Uwe na uhakika wa kuwapa Waisraeli nchi kama urithi, kama nilivyokuagiza. Igawanye nchi hii kama urithi kwa makabila tisa na kwa nusu ya kabila la Manase. Pamoja na nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi wamekwisha kupokea urithi wao ambao Musa aliwapa katika upande wa mashariki wa Yordani, kutoka Aroeri, iliyo katika ukingo wa bonde la mto Arnoni (kujumuisha na mji ambao uko katikati ya bonde), kwa nyanda zote za Medeba hadi Diboni; 10 miji yote ya Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala katika Heshiboni, hata mpaka wa Waamori, 11 Gileadi na mkoa wa Wageshuri na Maakathi, mlima wote wa Hermoni, Bashani yote mpaka Saleka; 12 ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyetawala katika Ashitarothi na Edrei - hawa ni wale waliosalia katika Refaimu - ambao Musa aliwapiga na kuwafukuzia mbali. 13 Lakini watu wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri wala Wamakathi. Badala yake, Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo. 14 Kabila la Lawi pekee halikupewa urithi na Musa. Urithi wao ni sadaka za Yahweh, Mungu wa Israeli, zilizotolewa kwa moto, kama Mungu alivyomwagiza Musa. 15 Musa aliwapa urithi kabila la Rubeni, ukoo kwa ukoo. 16 Miliki yao ilikuwa kutoka Aroeri, juu ya ukingo wa bonde la Mto Arnoni, na mji ulio katikati ya bonde, na nyanda zote za Medeba. 17 Wareubeni walipata pia Heshiboni, na miji yake yote zilizo katika uwanda, Diboni, na Bamathi Baali, na Bethi Baalimeoni, 18 na Yahazi, na Kedemothi, na Mefaathi, 19 na Kiriathaimu, na Sibuma, na Zerethishahari juu ya kilima cha bonde. 20 Wareubeni walipata pia Bethi Peori, miteremko ya Pisiga, Bethi Yeshimothi, 21 miji yote ya uwanda, na ufalme wote wa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa ametawala katika Heshiboni, ambaye Musa alikuwa amemshinda pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Zuri, Huri na Reba, wana wa mfalme wa Sihoni, ambao walikuwa wameishi katika nchi. 22 Pia, watu wa Israeli walimwua kwa upanga Baalam mwana wa Beori, ambaye alifanya mambo ya uaguzi, miongoni mwa wale waliowaua. 23 Mpaka wa kabila la Rubeni ni Mto Yordani; huu ndio mpaka wao. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Rubeni, uliotolewa kwa kila ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao. 24 Hiki ndicho Musa alilipa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo: 25 Himaya yao ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Waamoni, hadi Aroeri, iliyo mashariki mwa Raba, 26 kutoka Heshiboni hadi Ramathi - Mizipe na Betonimu, kutoka Mahanaimu mpaka himaya ya Debiri. 27 Katika bonde, Musa aliwapa Bethi -Haramu, Bethi - Nimra, Sukothi, na Zafoni, ufalme uliobakia wa Sihoni mfalme wa Heshiboni, pamoja na Yordani kama mpaka, katika sehemu za chini za mwisho wa Bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki ng'ambo ya Yordani. 28 Huu ni urithi wa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao. 29 Musa aliwapa urithi nusu ya kabila la Manase. Urithi uligawiwa kwa nusu ya kabila la watu wa Manase kutokana na kabila zao. 30 Miliki yao ilikuwa kutoka Mahanaimu, Bashani yote, ufalme wote wa mfalme Ogu wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini; 31 nusu ya Gileadi, na Ashitarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Miji hii iligawanywa kwa ukoo wa Makiri mwana wa Manase -nusu ya watu wa Makiri, walipewa kwa kila familia zao. 32 Huu ndio urithi ambao Musa aliowagawia katika nyanda za Moabu, ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko. 33 Musa hakulipa urithi kabila la Lawi. kwa kuwa Yahweh, Mungu wa israeli, ni urithi wao, kama vile alivyowaambia.