23
1 Na baada ya siku nyingi, kipindi ambacho Yahweh alikuwa ameipa Israeli pumziko kutoka maadui zao waliowazunguka,
2 Joshua alikuwa mzee sana. Yoshua aliwaita Waisraeli wote, na wazee wao, na viongozi, na waamuzi, na kwa maafisa, na kisha akawaambia, “Mimi nimezeeka sana.
3 Mmeshaona kila kitu ambacho Yahweh Mungu wenu ameshafanya kwa mataifa haya yote kwa ajili yenu, kwa kuwa ni Yahweh Mungu wenu ambaye amewapigania ninyi.
4 Tazama! Nimeshawakabidhi kwenu mataifa yaliyosalia ili kuyateka kwa ajili ya kupata urithi ya makabila yenu, sambasamba na mataifa yote ambayo tayari nimeshayaangamiza, tangu Yordani hadi Bahari kuu katika upande wa magharibi.
5 Yahweh Mungu wenu atayaondoa. Atayafukuzia mbali kutoka kwenu. Ataiteka nchi yao, nanyi mtaimiliki nchi yao, kama vile Yahweh Mungu wenu alivyowaahidi ninyi.
6 Hivyo, iweni jasiri, ili kwamba mtunze na kuyafanya yale yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa, msikengeuke upande wa kulia wala upande wa kushoto,
7 basi msichanganyikane na mataifa haya ambayo yamesalia miongoni mwenu, wala msiyataje majina ya miungu yao, wala msiape kwayo, wala msiiabudu, wala msiipigie magoti.
8 Badala yake, mnatakiwa kumshika sana Yahweh Mungu wenu kama vile mlivyofanya siku hii ya leo.
9 Kwa kuwa Yahweh ameyafukuzia mbali mbele yenu mataifa makubwa yenye nguvu. Hakuna hata mmoja aliyeweza kusimama mbele yenu hata siku hii ya leo.
10 Mtu yeyote mmoja wa kwenu atawafanya watu elfu wakimbie mbali, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ndiye anayepigania ninyi, kama vile alivyowaahidi.
11 Zingatieni kwa uangalifu ili mmpende Yahweh Mungu wenu.
12 Lakini kama mkiegeuka na kushikamana na watu walioalia wa mataifa haya waliobaki miongoni mwenu, au kuoana nao, au kama mkishirikiana pamoja nao, na wao pamoja nanyi,
13 jueni kwa hakika kwamba Yahweh Mungu wenu hatayafukuzia mbali mataifa haya yatoke kati yenu. Badala yake, watakuwa kitanzi na mtego kwenu, viboko migongoni mwenu na miiba machoni mwenu, mpaka pale mtakapoangamia katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
14 Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote, na mnajua kwa moyo na roho zenu zote kwamba hakuna hata neno moja ambalo halijatimia kati ya mambo yote mazuri ambayo Yahweh Mungu wenu aliyaahidi juu yenu. Vitu hivi vyote vimetokea kwa ajili yenu. Hakuna hata moja lililoshindikana.
15 Lakini kama kila neno ambalo Yahweh Mungu wenu alilowaahidi limekwisha kutimia, hivyo Yahweh atawaletea juu yenu mabaya yote mpaka pale atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
16 Atafanya hivi kama mtalivunja agano la Yahweh Mungu wenu, ambalo aliwaagizeni kulitunza. Kama mtaenda na kuiabudu miungu mingine na kuiinamia, ndipo hasira ya Yahweh itawaka kinyume nanyi, na ninyi mtaangamia upesi katika nchi nzuri ambayo amekwisha kuwapeni ninyi.”