13
1 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoazi mwana wa Yehu alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na saba.
2 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe na kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kuasi; na Yehoazi hakurudi kutoka kwao
3 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, na akaendelea kuwakabidhi kwenye mikono ya Hazaeli mfalme wa Shamu na kwenye mikono ya Ben Hadadi mwana wa Hazaeli.
4 Hivyo Yehoazi akamsihi Yahwe, na Yahwe akamsikiliza kwa sababu aliona mateso ya Israeli, vile mfalme wa Shamu alivyokuwa akiwatesa.
5 Basi Yahwe akawapa Israeli ulinzi, na wakakimbia kutoka kwenye mikono ya Washami, na watu wa Israeli wakaanza kuishi kwenye nyumba zao kama walivyokuwa kabla.
6 Hata hivyo, hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambaye alisabisha Israeli kuasi, na wakaendelea katika hayo; na huyo Ashera akabaki hivyo katika Samaria.
7 Washami wakamuacha Yehoazi pamoja na waendesha farasi hamsini tu, magari ya farasi kumi, na watembea kwa miguu elfu kumi, kwa ajili ya mfalme wa Shamu alikuwa ameiharibu na kuwafanya kama makapi yaliyopurwa.
8 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yehoazi, na yote aliyoyafanya na nguvu zake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
9 Basi Yehoyazi akalala na mababu zake, na wakamzika katika samaria. Yohoashi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.
10 Katika mwaka wa thelathini na saba wa Yoashi mfalme wa Yuda, utawala wa Yehoashi mwana wa Yehoazi ulianza juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na sita.
11 Akafanya yaliyo maovu kwenye uso wa Yahwe. Hakuacha nyuma dhambi zozote za Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa kuwa aliwafanya Israeli kuasi, lakini alitembea pamoja nao.
12 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoashi, na yote aliyoyafanya, na shujaa wake ambaye aliyepigana dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
13 Yehoashi akalala na mababu zake, na Yeroboamu akakalia kiti chake cha enzi cha kifalme. Yehoashi akazikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli.
14 Basi Elisha akaugua ugonjwa ambao baadae ulimuua, hivyo Yehoashi yule mfalme wa Israeli akashuka chini kwake na kumlilia juu yake. Akasema, “Baba yangu, baba yangu, haya magari ya farasi ya Israeli na hawa waendesha farasi wanakuchukua!”
15 Elisha akamwambia, “Chukua upinde na mishale,” basi Yoashi akachukua upinde na mishale.
16 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Weka mkono wako kwenye upinde,” basi akaweka mkono wake kwenye huo. Kisha Elisha akalaza mikono yake kwenye mikono ya mfalme.
17 Elisha akasema, “Fungua dirisha upande wa mashariki,” basi akalifungua. Kisha Elisha akasema, “Funga”, na akafunga. Elisha akasema, “Huu ndiyo mshale wa ushindi wa Yahwe, huu mshale wa ushindi juu ya Shamu, kwa kuwa utawapiga Washami katika Afeki hadi utakapowaangamiza.”
18 Kisha Elisha aksema, “Chukua mishale,” basi Yoashi akaichukua. Akamwambia mfalme wa Israeli, “Piga chini pamoja nao,” na akapiga chini mara tatu, kisha akaacha.
19 Lakini mtu wa Mungu alikuwa na hasira naye na akasema, “Ungelipiga chini mara tano au mara sita. Ndipo ungeipiga Shamu hadi kuiangamiza, lakini sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.”
20 Kisha Elisha akafa, na wakamzika. Sasa vikundi vya Wamoabi wakaingia kwenye nchi mwanzoni mwa mwaka.
21 Ikawa walipokuwa wakimzika huyo mtu, wakaona kundi la Wamoabi, hivyo wakautupia ule mwili kwenye kaburi la Elisha. Mara yule mtu alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama kwa miguu yake.
22 Hazaeli mfalme wa Shamu akawatesa Israeli siku zote za Yehoazi.
23 Lakini Yahwe aliwahurumia Israeli, na alikuwa na huruma juu yao na kushuhulika kwa ajili yao, kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Hivyo Yahwe hakuwaangamiza, na bado hakuwatupa kutoka kwenye uwepo wake.
24 Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, na Ben Hadadi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
25 Yehoashi mwana wa Yehoazi akairudisha kutoka kwa Ben Hadadi mwana wa Hazaeli miji ambayo aliichukua kutoka Yehoazi baba yake kwa vita. Yehoashi akamshambulia mara tatu, na akaipata miji ya Israeli.