20
Yahweh akazungumza na Musa, akasema, “Waambie watu wa Waisraeli, 'mtu yeyote miongoni mwa watu Israeli, au Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwa Waisraeli atakayemtoa mtoto wake yeyote kwa Moleki, hakika atauawa. Ni lazima watu wa nchi wamponde kwa mawe. Pia nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake kwa sababu amemtoa mtoto wake kwa Moleki, ili kupatia unajisi mahali pangu patakatifu na kulinajisi jina langu takatifu. Na kama watu wa nchi watayafumba macho yao kwa mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa Moleki, kama hawatamwua mtu huyo, ndipo Mimi mwenyewe nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na ukoo wake, Nami nitamkatilia mbali pamoja na yeyote anayejifanya kahaba ili kufanya umalaya na Moleki. Mtu yule anayewageukia wanaozungumza na wafu, au na wale wanaozungumza na roho ili kufanya ukahaba nao, Nitakaza uso wangu dhidi ya mtu huyo; Nami nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake. Kwa hiyo jitakaseni wenyewe na muwe watakatifu, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu. Mtazitunza amari zangu na kuzifuta. Mimi ndimi Yahweh anayewatenga ninyi muwe watakatifu. Yeyote amlaaniye baba yake au mama yake hakika mtu huyo atauawa. Amemlaani baba yake au mama yake, kwa hiyo ana hatia na anastahili kufa. 10 Mwanaume yeyote afanyaye uzinzi na mke wa mwanaume mwingine, yaani, yeyote anayezini na mke wa jirani yake—yule mwanaume mzinzi na mwanamke mzinzi ni lazima wote wawili wauawe. 11 Mwanaume yeyote anayelala na mke wa baba yake ili kukutana naye kimwili amemfedhehesha baba yake mwenye. Wote wawili; mwana huyo na mke huyo wa baba yake kwa hakika watauawa. wanahatia na wanastahili kufa. 12 Kama mwanaume atalala na mke wa mwanawe, wote wawili; mwanaume huyo na mke huyo wa mwanawe hakika watauawa. Wametenda upotovu. Wana hatia na wanastahili kufa. 13 Kama mwanaume analala na mwanaume mwingine kama alalavyo na mwanamke, wote wawili watakuwa wamefanya jambo lililo ovu. Hakika watauawa. Wana hatia na wanastahili kufa. 14 Ikiwa mwanaume atamwoa mwanamke na pia akamwoa mama wa mwanamke huyo, huu ni uovu. Ni lazima wachomwe kwa moto, wote wawili, mwanaume huyo na manamke huyo, ili kwamba hapatakuwepo na uovu miongoni mwenu. 15 Ikiwa mwanaume analala na mnyama, hakika atauawa, ni lazima mumuue na mnyama huyo pia. 16 Ikiwa mwanamke anamkaribia mnyama ili kulala naye, ni lazima mmuuwe mwanamke huyo pamoja na mnyama. Kwa hakika ni lazima wauawe. wana hatia na wanastahili kufa. 17 Ikiwa mwanaume analala na dada yake, ama ni binti ya baba yake au binti ya mama yake—ikiwa wamelala pamoja, hilo ni jambo la aibu. Ni lazima wakatiliwe mbali watoke machoni pa watu wao, kwa sababu amelala na dada yake. Ni lazima aibebe hatia yake. 18 Kama mwanaume analala na mwanamke katika kipindi cha hedhi yake, na amekutana naye kimwili, atakuwa amefunua mtiririko wa damu yake, chanzo cha damu yake. Ni lizima wote wawili wakatiliwe mbali kutoka mingoni mwa watu wao. 19 Usilale na dada ya mama yako, au dada ya baba yako, kwa sababu ungeweza kumwaibisha jamaa yako wa karibu. Ni lazima utabeba hatia yako mwenyewe. 20 Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao. 21 Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote amabayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao. 22 Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi. 23 Msienende katika desturi za mataifa ambayo nitayafukuza mbele yenu, ni kwa sababu wamefanya mambo haya yote, nami mimewachukia wao. 24 Nami nikawaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao, nitaitoa kwenu ili muimiliki, nchi itiririkayo amaziwa na asali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine. 25 Ni lazima pia mtofautishe kati ya wanya najisi na wale walio safi, na kati ya ndege walio najisi na walio safi. Msijichafue wenyewe kwa wanyama au ndege au kiumbe kitambaacho juu ya nchi kilicho najisi, ambacho nimekitenga kuwa najisi. 26 Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi, Yahweh, ni mtakakatifu, nami nimewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine, kwa kuwa nyinyi ni wangu. 27 Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.