9
1 Katika siku ya nane, Musa akawaita Aroni na wanawe pamoja na wazee wa Israeli.
2 Akamwambia Aroni, “Twaa ndama dume kutoka kundini kwa ajili ya sadaka ya dhambi zako, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, na uwatoe mbele za Yahweh.
3 Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Twaeni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi na ndama na mwana-kondoo, hawa wawili wawe na umri wa mwaka mmoja na bila dosari, ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
4 pia twaeni fahali na kondoo dume kwa sadaka za amani ili kuwatoa mbele za Yahweh, na sadaka za nafaka iliyochanganywa na mafuta, kwa sababu leo Yahweh atajidhihirisha kwenu.
5 Kwa hiyo wakaleta kwenye hema la kukutania vyote ambavyo Musa aliagiza, nalo kusanyiko lote la Israeli likakaribia na kusimama mbele za Yahweh.
6 Kisha Musa akasema, “Hivi ndivyo Yahweh amewaamru nyinyi mfanye, ili kwamba utukufu wake uweze kuonekana kwenu.
7 “Musa akamwambia Aroni, “Njoo karibu na Madhabahu na uteo sadaka yako ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu ili kufanya upatanisho kwa ajili yao kama vile ambavyo Yahweh amekwishaamru.”
8 Kwa hiyo Aroni akaikaribia madhabahu na akamchinja yule ndama kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ambayo ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe.
9 Nao wana wa Aroni wakamletea hiyo damu, naye akakichofya kidole chake kwenye damu na kuiweka kwenye pembe za madhabahu, kisha akaimwaga damu chini ya kitako cha madhabahu.
10 Hata hivyo, aliyateketeza hayo mafuta, figo, na mafuta yanafunika ini juu ya madhabahu kuwa sadaka ya dhambi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
11 Na akaiteketeza hiyo nyama pamoja na ngozi nje ya kambi
12 Aroni akaichinja sadaka ya kuteketezwa, nao wanawe wakampa hiyo damu, ambayo aliinyunza pande zote za madhabahu.
13 Kisha wakampa ile sadaka ya kuteketezwa, kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.
14 Akaziosha sehemu za ndani pamoja na miguu na kuziteketeza juu ya dhabihu ya kuteketezwa juu ya Madhabahu.
15 Aroni akaleta dhabihu ya watu— mbuzi, kisha akamtoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi yao naye akamchinja, akaitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi, kama alivyofanya kwa yule mbuzi wa kwanza.
16 Akaileta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama Yahweh alivyokuwa ameamru.
17 Akaileta sadaka ya nafaka; akakijaza kiganja chake nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa.
18 Pia akamchinja fahali na yule kondoo dume, dhabihu kwa ajili ya sadaka ya amani, ambayo ilikuwa kwa ajili ya watu. Nao wana wa Aronni wakampa damu, ambayo aliinyunyiza kila upande wa mdhabahu.
19 Hata hivyo, waliyakata mafuta ya fahali na ya yule kondoo dume, mafuta ya kwenye mkia, mafuta yafunikayo sehemu za ndani, figo, na yale mafuta yaliyofunika mapafu.
20 Wakazichukua hizi sehemu zilizokatwa wakaziweka juu ya vidari, na kisha Aroni akateketeza mafuta juu ya madhabahu.
21 Naye Aroni akavitikisa vidari na paja la kulia kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh, kama vile Musa alivyokuwa ameamru,
22 Kisha Aroni akainua juu mikono yake mbele ya watu na kuwabariki, kisha akashuka chini kutoka mahali alipokuwa akitoa hiyo sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani.
23 Musa na Aroni wakaingia ndani ya hema la kukutania, kisha wakatoka nje tena na kuwabariki watu, na utukufu wa Yahweh ukaonekana kwa watu wote.
24 Moto ukashuka kutoka kwa Yahweh na ukairamba sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wlipoona jambo hili, wakapiga kelele na kulala chini.