3
1 Nimesema'”Sasa sikilizeni, ninyi viongozi wa Yakobo na kutawala nyumba ya Israeli: Je siyo sahihi kwenu kuielewa haki?
2 Ninyi manaochukia mazuri na kupenda uovu, ninyi mnaoambua ngozi yao, miili yao kutoka kwenye mifupa yao-
3 ninyi mnaokula pia miili ya watu wangu, na kuambua ngozi yao, kuvunja mifupa yao, na kuwakatakata katika vipande vipande, kama nyama kwenye chungu, kama nyama kwenye sufuria kubwa.
4 Kisha ninyi watawala mtalia kwa Yahwe, lakini hatawajibu. Atauficha uso wake kutoka kwenu kipindi hicho, kwasababu mmefanya matendo maovu.”
5 Yahwe asema hivi kuhusu manabii ambao wawafanyao watu wangu kushindwa, “Kwa wale wawalishao wanatangaza, 'Kutakuwa na ustawi.' Lakini kwa wale wasioweka kitu kwenye vinywa vyao, wanaanzisha vita dhidi yake.
6 Kwa hiyo, itakuwa usiku kwenu usiokuwa na maono juu yenu; itakuwa giza ili kwamba msiweze kubashiri. Jua litakwenda chini juu ya manabii, na siku itakuwa giza juu yao.
7 Waonaji watawekwa kwenye aibu, waaguzi wa watachanganyikiwa. Wote watafunga midomo yao, kwa kuwa hakuna jibu kutoka kwangu.”
8 Lakini kwangu, nimejazwa nguvu kutoka kwa Roho wa Yahwe, na nimejaa haki na uweza, kumwambia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
9 Sasa sikieni hii, ninyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, na watawala wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao mnaochukia haki, na kupotosha kila haki.
10 Mnaijenga Sayuni kwa damu na Yerusalemu kwa uovu.
11 Viongozi wenu huhukumu kwa rushwa, makuhani wenu hufundisha kwa hijara, na manabii wenu hufanya utabiri kwa ajili ya pesa. Hata hivyo bado mtamtegemea Yahwe na kusema, “Je hayupo Yahwe pamoja nasi? Hakuna uovu utakaokuja juu yetu.”
12 Kwa hiyo, kwasababu yenu, Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa rundo la kifusi, na mwinuko wa hekalu utakuwa kama mwinuko wa msituni.