12
1 Hawa ndio makuhani na Walawi waliokuja pamoja na Zerubabeli mwana wa Shealueli, pamoja na Yoshua Seraya, Yeremia, Ezra,
2 Amaria, Maluki, Hatushi,
3 Shekania, Harimu na Meremothi.
4 Kulikuwa na Iddo, Ginethoni, Abiya,
5 Miyamini, Maazia, Bilgai,
6 Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,
7 Salu, Amoki, Hilkia, na Yedaya. Hawa walikuwa wakuu wa makuhani na washirika wao katika siku za Yoshua.
8 Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa akiongoza nyimbo za shukrani, pamoja na washirika wake.
9 Bakbukia na Uno, washirika wao, walisimama pembeni yao wakati wa huduma.
10 Yoshua alikuwa babaye Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa babaye Yoyada,
11 Yoyada alimzaa Yonathani, Yonathani akamzaa Yadua.
12 Katika siku za Yoyakimu hawa walikuwa makuhani, wakuu wa jamaa; Meraya alikuwa mkuu wa Seraya, Hanania alikuwa kiongozi wa Yeremia,
13 Meshulam alikuwa kiongozi wa Ezra, Yehohanani alikuwa kiongozi wa Amaria,
14 Yonathani alikuwa kiongozi wa Maluki, na Yusufu alikuwa kiongozi wa Shekania.
15 Ili kuendelea, Adna alikuwa kiongozi wa Harimu, Helkai kiongozi wa Meremothi,
16 Zekaria alikuwa kiongozi wa Ido, Meshulamu alikuwa kiongozi wa Ginethoni, na
17 Zikri alikuwa kiongozi wa Abia wa Miyaamini. Piltai alikuwa kiongozi wa Maazia.
18 Shamua alikuwa kiongozi wa Bilgai, Yehonathani alikuwa kiongozi wa Shemaya,
19 Matenai alikuwa kiongozi wa Yoyaribu, Uzi alikuwa kiongozi wa Yedaya,
20 Kalai alikuwa kiongozi wa Salu, Eberi alikuwa kiongozi wa Amok,
21 Hashabia alikuwa kiongozi wa Hilkia, na Nethanel alikuwa kiongozi wa Yedaya.
22 Katika siku za Eliashibu, Walawi Eliashibu, Yoyada, Yohana, na Yadua waliandikwa kama vichwa vya familia, na makuhani waliandikwa wakati wa utawala wa Dariyo wa Persia.
23 Wana wa Lawi na viongozi wao wa familia waliandikwa katika Kitabu cha tarehe hadi siku za Yohana mwana wa Eliashibu.
24 Wakuu wa Walawi walikuwa Hashabia, Sherebia, na Yeshua mwana wa Kadmieli, pamoja na washirika wao, waliokuwa wamesimama mbele yao kumtukuza na kumshukuru, akijibu sehemu kwa sehemu, kwa kutii amri ya Daudi, mtu wa Mungu.
25 Matania, Bakbukia, Obadiya, Meshulamu, Talmoni na Akubu walikuwa walinzi wa malango waliokuwa wakiwa wamesimama katika vyumba vya hazina penye malango.
26 Walitumika katika siku za Yoyakimu, mwana wa Yoshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za Nehemiya, gavana na Ezra kuhani na mwandishi.
27 Katika kujitolea kwa ukuta wa Yerusalemu, watu walitafuta Walawi popote walipokuwa wakiishi, wakawaleta Yerusalemu ili kusherehekea kujitolea kwa furaha, pamoja na shukrani na kuimba kwa ngoma, vinanda na vinubi.
28 Ushirika wa waimbaji walikusanyika pamoja kutoka wilaya iliyozunguka Yerusalemu na kutoka vijiji vya Wanetofathi.
29 Walikuja kutoka Beth-gilgali na kutoka katika mashamba ya Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji karibu na Yerusalemu.
30 Makuhani na Walawi wakajitakasa, kisha wakawatakasa watu, milango na ukuta.
31 Kisha nilikuwa na viongozi wa Yuda kwenda juu ya ukuta, na mimi kuteua mikutano miwili mikubwa ya hao walioshukuru. Mmoja alienda upande wa kulia juu ya ukuta kuelekea lango la jaa.
32 Hoshaya na nusu ya viongozi wa Yuda walimfuata,
33 na baada yake akaenda Azaria, Ezra na Meshulamu,
34 Yuda, Benyamini, Shemaya, Yeremia
35 na wana wa makuhani waliokuwa na tarumbeta, na Zekaria mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Mataniya, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu.
36 Na pia jamaa za Zekaria, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, Hanani, pamoja na vyombo vya muziki vya Daudi mtu wa Mungu. Ezra mwandishi alikuwa mbele yao.
37 Na kwa Lango la Chemchemi walikwenda moja kwa moja na madaraja ya mji wa Daudi juu ya kupanda kwa ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, kwenye lango la Maji upande wa mashariki.
38 Na waimbaji wengine ambao walishukuru wakaenda upande mwingine. Niliwafuata juu ya ukuta pamoja na nusu ya watu, juu ya mnara wa vinyago, hadi kuta kubwa,
39 na juu ya lango la Efraimu, na mlango wa kale, na kwa lango la samaki na mnara wa Hananeli na mnara wa Hamea, kwa lango la Kondoo, na wakasimama kwenye mlango wa walinzi.
40 Kwa hiyo, mikutano miwili ya wale waliomshukuru walipata nafasi yao katika nyumba ya Mungu, na mimi pia nikachukua nafasi yangu na nusu ya viongozi pamoja nami.
41 Na makuhani wakachukua nafasi zao Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria, na Hanania wenye tarumbeta,
42 Maaseya, na Shemaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu, Ezeri. Waimbaji waliimba na Yezrahia kama wasimamizi.
43 Walitoa dhabihu kubwa siku ile, wakafurahi, kwa sababu Mungu alikuwa amewafurahisha kwa furaha kubwa. Pia wanawake na watoto walifurahi. Hivyo furaha ya Yerusalemu ikasikiwa toka mbali.
44 Siku hiyo watu waliteuliwa juu ya nyumba ya hazina kwa ajili ya michango, matunda ya kwanza, na zaka, ili kuzikusanya ndani yao sehemu zinazohitajika katika sheria za makuhani na Walawi. Kila mmoja aliteuliwa kufanya kazi mashambani karibu na miji. Kwa maana Yuda alifurahi juu ya makuhani na Walawi waliokuwa wamesimama mbele yao.
45 Walifanya utumishi wa Mungu wao, na huduma ya utakaso, kwa mujibu wa amri ya Daudi na ya mwanawe Sulemani, na hivyo
46 Zamani za kale, katika siku za Daudi na Asafu, kulikuwa na wasimamizi wa waimbaji, na kulikuwa na nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu.
47 Katika siku za Zerubabeli na katika siku za Nehemia, Israeli wote walitoa sehemu za kila siku kwa waimbaji na walinzi wa mlango. Wakaweka pembeni sehemu ya Walawi, na Walawi waliweka sehemu ya wana wa Haruni.