17
1 BWANA akanena na Musa, akasema,
2 “Waambie wana wa Israeli wakuletee fimbo za kutembelea moja kwa kila jamaa, fimbo kumi na mbili. Uandika jina la kila mmoja kwenye hizo fimbo.
3 Utaandika jina la Haruni kwenye jina la Lawi. Kutakuwa na fimbo moja kwa kila kiongozi kutoka kwenye kabila la mababu zake.
4 Utaziweka hizo fimbo kwenye hema ya kukutania mbele ya amri za agano, ambapo Mimi hukutana na wewe. Itakuwa hivi,
5 fimbo ya mtu yule ninayemchagua itachipua. Nitazuia watu wa Israeli walalamikao, ambao wanaongea kinyume na wewe.”
6 Kwa hiyo Musa akawaambia wana wa Israeli. Viongozi wote wa kabila wakampatia fimbo, fimbo moja kutoka kwa kila kiongozi, aliyechaguliwa kutoka kwenye kila kabila ya babu zao, jumla yake fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Haruni ilikuwa miongoni mwa fimbo hizo.
7 Ndipo Musa alipoziweka zile fimbo mbele ya BWANA katika hema ya amri ya agano.
8 Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye hema ya amri ya agano, na tazama, fimbo ya Haruni kwa ajili ya Kabila la Lawi ilikuwa imetoa machipukizi. Machipukizi yalikuwa hadi kuchanua maua na kuzaa malozi mabivu!
9 Musa akazitoa fimbo zote kutoka kwa BWANA kwa watu wote wa Israeli, na kila mtu akachukua fimbo yake.
10 BWANA akamwambua Musa, “Iweke fimbo ya Haruni mbele ya amri za agano. Iweke iwe ishara ya hatia mbele ya watu waliopinga ili ukomeshe malalamiko dhidi yangu, vinginevyo watakufa.”
11 Musa akafanya kama BWANA alivyoagiza.
12 Wana wa Israeli wakanena na Musa wakisema, “tutakufa hapa! Wote tutaangamia!
13 Kila mmoja anayekuja hapa, anayekaribia masikani ya BWANA, atakufa. Je, ni lazima wote tuangamie?”