5
1 BWANA alinena na Musa. Akasema,
2 “Waamuru wana wa Israel wawatoe watu wote wenye magonjwa ya ngozi yanayoambukiza, na kila mwenye mwenye vidonda vinavyotoa harufu, na ambaye amenajisika kwa kugusa maiti.
3 Awe mme au mke, umtoa kambini. Ili wasije wakaitia unajisi kambi, kwa sababu Mimi huishi ndani yake,”
4 Watu wa Israeli walifanya hivyo. Waliwatoa kambini, Kama BWANA alivyomwagiza Musa. Watu wa Israeli walimtii BWANA.
5 Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,
6 “Nena na wana wa Israeli. mtu mume na mtu mke akifanya dhambi yeyote ambayo watu hufanyiana wao kwa wao, na mtu huyo akamwasi BWANA, mtu huyo atakuwa na hatia.
7 Ndipo huyo mtu ataungama hiyo dhambi aliyoifanya. Mtu huyo atarudisha malipo ya hatia yake na kuongeza kwenye malipo hayo sehemu ya tano zaidi. Atamlipa huyo aliyemtendea makosa
8 Lakini kama huyo mtu huyu aliyetendewa kosa hana ndugu wa kupokea hayo malipo, basi atalipa hayo malipo ya hatia kwangu kupitia kuhani pamoja na kondoo dume kwa ajili ya sadaka yake mwenyewe.
9 Kila sadaka ya wana wa Israeli, vitu ambavyo vimetengwa na vikaletwa kwa kuhani na watu wa Israeli, vitakuwa vyake.
10 Sadaka ya kila mtu itakuwa ya kuhani; kama mtu yeyote atatoa kitu chochote kwa kuhani, kitakuwa chake.”
11 Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,
12 “Nena na wana wa Israel. Uwaambie, 'kama mke wa mtu ataasi na kufanya dhambi dhidi ya mume wake.
13 Halafu mtu mwingine akalala naye. Kwa sababu, hiyo atakuwa amenajisika. Na hata kama mume wake hakuona na hajui, hata kama hakuna mtu aliyemkamta akiwa katika tendo na hakuna mtu wa kushuhudia dhidi yake; hata hivyo ile roho ya wivu itaendele kumjulisha yule mume kuwa mke wake amenajisika.
14 Ingawa, roho ya wivu inaweza kumdanganya yule mwanamume wakati mke wake hajanajisika.
15 Kwa mazingira hayo, yule mwanamume anapaswa kumpeleka mke wake kwa kuhani. Yule mwanamume anapaswa kutoa sadaka ya divai kwa ajili yake. Atapaswa kuleta sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri. Asitie mafuta juu yake wala asitie ubani juu yake maana ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho wa uovu.
16 Ndipo kuhani atasogeza karibu na kumweka mbele ya BWANA.
17 Kuhani atachukua kikombe cha maji matakatifu na atachukua mavumbi ya kwenye masikani. Ataweka yale mavumbi kwenye maji.
18 Kisha kuhani atamweka huyo mwanamke mbele za BWANA na atazifungua nywele kichwani kwa huyo mwanamke. Atamwekea mikononi mwake hiyo sadaka ya unga kwa ajili ya ukumbusho, ambayo ni sadaka ya unga kwa ajili ya wivu.
19 Kuhani atashikilia mikononi mwake maji machungu yanayoweza kuleta laana. Kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya kiapo na kumwambia. 'Kama haujafanya uzinzi na mwanaume mwingine, na kama hajakengeuka na kufanya uovu, basi utakuwa huru na maji haya yanayoweza kuleta laana.
20 Lakini kama wewe, mwanamke uliye chini ya mume wako, umekengeuka, na kama umenajisika, na kama mwanamume mwingina amelala nawe,
21 ndipo, (kuhani atamtaka huyo mwanamke aape kiapo kinachoweza kuleta laana kwake, na kwamba ataendelea kumwambia yule mwanamke) 'BWANA atakufanya wewe kuwa laana itakayooneshwa kuwa hivyo kwa watu wako. Hii itatokea pale BWANA atakapoyafanya mapaja yako kuoza na tumbo lako kuvimba.
22 Haya maji ambayo huleta laana yataingia tumboni mwako na kulifanya tumbo lako kuvimba na mapaja yako kuoza,' mwanamke alitakiwa kujibu, 'Ndiyo, hayo yanipate kama mimi ni mwenye hatia.'
23 Naye kuhani ataziandika laana hizi kwenye kitabu, na kisha kuzifuta laana zilizoandikwa kwa maji ya uchungu.
24 Naye kuhani atamwelekeza yule mwanamke kunywa yale maji machungu yaletayo laana. Yale maji yaletayo laana yataingia na kuwa machungu.
25 Kuhani ataitwaa ile sadaka ya unga ya wivu mikononi mwa yule mwanamke. Atailekeza ile sadaka ya unga mbele ya BWANA na kuileta madhabahuni.
26 Kuhani atachukua konzi ya sadaka ya unga mkononi mwake kama sadaka ya kuwakilisha, na kuiteketeza madhabahuni. Ndipo atakapompatia mwanamke yale maji machungu ili ayanywe.
27 Wakati wa kumpa yale maji ili anywe, kama amenajisika kwa sababu alifanya uovu dhidi ya mume wake, ndipo yale maji yaletayo laana yatamwingia na kuwa machungu. Tumbo lake litavimba na paja lake litaoza. Yule mwanamke atalaaniwa kati ya watu wake.
28 Lakini kama yule mwanake hajanajisika na kama ni msafi, basi atakuwa huru. Tena ataweza kubeba uja uzito.
29 Hii ndiyo sheria ya wivu. Ni sheria ya mwanamke anayekengeuka kwa mumewe na kunajisika.
30 Ni sheria ya mwanamume mwenye roho ya wivu kwa mkewe. Atamleta mwanamke mbele ya BWANA, na kuhani atamfanyia huyo mwanamke kila kitu ambacho sheria ya wivu inamtaka kufanya.
31 Yule mwanamume atakuwa hana hatia kwa kumleta mke wake kwa kuhani. Na yule mwanmke atauchukua uovu wake.”