7
1 Mwanangu, yatunze maneno yangu na ndani yako udhihifadhi amri zangu.
2 Uzilinde amri zangu ili uishi na uyatunzetu mafundisho yangu kama mboni ya jicho.
3 Uyafunge katika vidole vyako; uyaandike katika kibao cha moyo wako.
4 Mwambie hekima, “wewe ni dada yangu,” na ufahamu mwite jamaa yako,
5 ili ujitunze mwenyewe dhidi ya mwanake haramu, dhidi ya mwanamke mgeni mwenye maneno laini.
6 Nilikuwa naangalia kwenye wavu wa dirisha la nyumba yangu.
7 Nikawatazama watu mwenye ukosefu wa uzoefu, na miongoni mwa watu vijana nikamwona kijana asiye na akili.
8 Kijana huyo alishuka mtaani kwenye kona karibu na yule mwanamke, akaenda kwenye nyumba yake.
9 Ilikuwa katika utusiutusi wa siku muda wa jioni, wakati wa usiku na giza.
10 Akakutana na yule mwanake, amevaa kama kahaba, katika moyo wa udanyanyifu.
11 Alikuwa na kelele na upotovu; miguu yake haikutulia kwenye masikani.
12 Alielekea mitaani, kisha sehemu ya sokoni, na katika kila upande alisubiri kwa kuviza.
13 Basi akamshika na kumbusu, kwa uso wa nguvu akamwambia,
14 leo nimetoa sadaka yangu ya amani, nimelipa nadhili yangu,
15 hivyo nilikuja kukutana nawe, kuutafuta uso wako kwa hamu, na sasa nimekupata.
16 Nimeweka matandiko juu ya kitanda changu, kitani za rangi kutoka Misri.
17 Kitanda changu nimenyunyizia manemane, udi na mdalasini.
18 Njoo, tunywe tujishibishe kwa upendo wetu hata asubuhi; tupate furaha kuu kwa matendo ya mahaba.
19 Maana mume wangu hayupo nyumbani kwake; amekwenda safari ya mbali.
20 Alichukua mkoba wa fedha; atarudi siku ya mwezi mpevu.
21 katika maneno yake mengi akamshinda; na kwa midomo yake laini anampotosha.
22 Ghafula alimfuata kama maksai anayekwenda kwa mchinjaji, kama ayala aliyekamatwa kwa nguvu,
23 mpaka mshale upasue ini lake. Alikuwa kama ndege anayekimbili kwenye mtego. Hakujua kuwa itamgharimu maisha yake.
24 Na sasa, wanangu, nisikilizeni; zingatieni maneno ya kinywa changu.
25 Moyo wako usiyageukie mapito yake; usipotoshwe katika mapito yake.
26 Amesababisha watu wengi kuanguka kwa kuwajeruhi; ameua watu wengi.
27 Nyumba yake ipo juu ya barabara ya kwenda kuzimu; huelekea chini kwenye vyumba vya mauti.