133
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Tazama, jinsi ilivyo vema na yakupendeza ndugu waishi pamoja, kwa umoja! Ni kama mafuta mazuri kichwani yashukayo ndevuni. Ndevu za Haruni, na yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Ni kama umande wa Hermoni uangukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko Bwana alipoamuru baraka, naam uzima milele na milele.