145
Zaburi ya sifa. Ya Daudi.
1 Nitakutukuza wewe, Mungu wangu, Mfalme; nitalihimidi jina lako milele na milele.
2 Kila siku nitakuhimidi; nitalisifu jina lako milele na milele.
3 Yahwe ndiye mkuu na wakusifiwa sana; ukuu wake hauchunguziki.
4 Kizazi kimoja kitayasifu matendo yako kwa kizazi kijacho na kitatangaza matendo yako makuu.
5 Nitaitafakari fahari ya utukufu wa adhama yako na matendo yako ajabu.
6 Watanena juu ya nguvu ya kazi zako za kutisha, nami nitatangaza ukuu wako.
7 Nao watatangaza wingi wa wema wako, na wataimba kuhusu haki yako.
8 Yahwe ni wa neema na huruma, si mwepesi wa hasira na mwingi katika uaminifu wa agano lake.
9 Yahwe ni mwema kwa wote; huruma zake zi juu ya kazi zake zote.
10 Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe.
11 Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako.
12 Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13 Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi.
14 Yahwe huwategemeza wote waangukao na huwainua wote walioinama chini.
15 Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi.
16 Huufungua mkono wako na hukidhi haja ya kila kiumbe hai.
17 Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo.
18 Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.
19 Hutimiza haja za wale wanao mheshimu yeye; husikia kilio chao na kuwaokoa.
20 Yahwe huwalinda wale wampendao, lakini atawaangamiza waovu wote.
21 Kinywa changu kitazinena sifa za Yahwe; wanadamu wote na walitukuze jina lake takatifu milele na milele.