2
Kwa nini mataifa wanafanya dhoruba, kwa nini watu wanafanya njama ambazo zitafeli? Wafalme wa nchi kwa pamoja hushikilia misimamo yao na watawala kwa pamoja hufanya njama kinyume na Yahwe na kinyume na Masihi, wakisema, “Ngoja tuzikate pingu walizo tufingia sisi na kuzitupa pingu zao.” Yeye aketie katika mbingu atacheka kwa dharau mbele yao; Bwana atawadhihaki wao. Kisha ataongea nao katika hasira yake na kuwaogofya kwa gadhabu yake, akisema, “Mimi mwenyewe nilimpaka mafuta mfalme wa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” Nami nitatangaza amri ya Yahwe. Yeye aliniambia, “wewe ni mwanangu! Leo hii nimekuwa baba yako. Uniombe, nami nitakupa wewe taifa kwa ajili ya urithi na mikoa ya nchi iliyo bora kwa ajili ya umiliki wako. Wewe utawavunja wao kwa fimbo ya chuma; kama vile mtungi wa mfinyanzi, wewe utawavunja wao vipande vipande.” 10 Hivyo sasa, ninyi wafalme; mchukue tahadhari; mjirekebishe. 11 Mwabuduni Yahwe kwa hofu na mfurahi mkitetemeka. 12 Mumbusu mwana vinginevyo atawakasirikia, na mtakufa pale pale hasira yake ikiwaka. Ni jinsi gani wamebarikiwa wale wote watafutao usalama ndani yake.