20
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mungu akusaidie wakati wa shida; na jina la Mungu wa Yakobo likulinde na kutuma msaada kutoka mahali patakatifu kwa ajili ya kukutegemeza wewe kutoka Sayuni. Naye akumbuke sadaka yako yote na kuipokea sadaka ya kuteketezwa. Naye akujalie haja za moyo wako na kutimiza mipango yako yote. Ndipo tutakapo shangilia katika ushindi wako, na, katika jina la Mungu wetu, tutapeperusha bendera. Yahwe naakupe maombi yako yote ya haki. Sasa ninajua ya kuwa Yahwe atawaokoa wapakwa mafuta wake; yeye atamjibu yeye kutoka katika mbingu takatifu kwa uweza wa mkono wake wa kuume ambao waweza kumuokoa yeye. Baadhi hamini katika magari na wengine katika farasi, lakini sisi tumuita Yahwe Mungu wetu. Wao watashushwa chini na kuanguka, bali sisi tutainuka na kusimama wima! Yahwe, umuokoe mfalme; utusaidie sisi tukuitapo.