24
Zaburi ya Daudi. Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia! Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe, mwenye nguvu na uweza; Yahwe, mwenye uweza katika vita. Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia! 10 Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe wa majeshi, yeye ni Mfalme wa utukufu.