29
Zaburi ya Daudi. Mpeni sifa Yahwe, enyi wana wa Mungu! Mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu. Mpeni Yahwe utukufu ambao jina lake linastahili. Mpigieni magoti Yahwe katika mapambo ya utakatifu. Sauti ya Yahwe imesikika zaidi ya maji; Mungu wa radi ya utukufu, radi yaYahwe i juu ya maji mengi. Sauti ya Yahwe ina nguvu; sauti ya Yahwe ni kuu. Sauti ya Yahwe huivunja mierezi; Yahwe huivunja vipande vipande mierezi ya Lebanon. Yeye huifanya Lebanoni kuruka kama ndama wa ng'ombe na Sirioni kama mwana wa nyati. Sauti ya Yahwe hutoa miale ya moto. Sauti ya Yahwe hutetemesha Jangwa; Yahwe hutetemesha jangwa la Kadeshi. Sauti ya Yahwe huufanya miti mikubwa kutikisika na huipukutisha misitu. Kila mmoja katika hekalu lake husema, “Utukufu!” 10 Yahwe hukaa kama mfalme juu ya mafuriko; Yahwe hukaa kama mfalme milele. 11 Yahwe huwatia nguvu watu wake; Yahwe huwa bariki watu wake na amani.