54
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Maschil ya Daudi; wakati Ziphites alipokuja na kumwambia Sauli, “Hivi Daudi hakujificha pamoja nasi?” Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu. Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu. Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. Selah Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye. Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu! Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema. Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.