87
Zaburi ya wana wa Kora; wimbo. Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu; Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo. Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'” Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha. Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”