12
1 Hawa walikuwa wanaume walio kuja kwa Daudi huko Zikilagi, wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa Sauli mwana wa Kishi. Walikuwa miongoni mwa wanajeshi, wasaidizi wake katika mapambano.
2 Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde. Walikuwa Wabenjamini, ndugu wa kabila moja na Sauli.
3 Kiongozi alikuwa Ahi Eza, halafu Yoashi, Wana wote wa Shemaa Mgibeathi. Kulikuwa na Yezieli na Peleti, wana wa Azimavethi. Kulikuwa pia na Beraka, Yehu Waanathothi,
4 Ishimaia Mgibeoni, mwanajeshi kati ya wale thelathini ( na kiongozi wa wale thelathini); Yeremia, Yahazieli, Yohana, Yozabadi Wagederathi,
5 Eluzai, Yerimothi, Bealia, Shemaria, Shefatia Waharufi,
6 Wakorahi ni Elkana, Ishia, Azareli, Yoeza, Yashobeamu, na
7 Yoela na Zebadia, wana wa Yeroham wa Gedori.
8 Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa wanaume wapiganaji, waliofundishwa kwa mapambano, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesi kwenye milima kama swala.
9 Kulikuwa na Eza kiongozi, Obadia wapili, Eliabu watatu,
10 Mishimana wanne, Yeremia watano,
11 Atai wasita, Elieli wasaba,
12 Yohana wanane, Elizabadi watisa,
13 Yeremia wakumi, Makibanai wakumi na moja.
14 Wana wa Gadi walikuwa viongozi wa jeshi. Wamwisho aliongoza mia moja, na mkubwa aliongoza elfu moja.
15 Walikatisha Yordani kwa mwezi wa kwanza, wakati vijito vyake vilipofurika, na kuwafukuza wote wanaoishi katika mabonde, pande zote za mashariki na magharibi.
16 Baadhi ya wanaume wa Benjamini na Yuda walikuja kwenye ngome kwa Daudi.
17 Daudi alienda nje kuwasalimu na kuwahutubia: “kama mmekuja kwa amani kunisaidia, mnaweza kujiunga nami. Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa maadui zangu, Ee Mungu wa mababu zetu awaone na kuwakemea, tangu sijafanya kosa.”
18 Kisha roho ikaja juu ya Amasai, ambaye alikuwa kiongozi wa wale thelathini. Amasai alisema, “Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse. na amani iwe juu ya yeyote atakaye kusaidia. Kuwa Mungu wako anakusaidia.” Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakuu wa watu wake.
19 Baadhi kutoka kwa Manase pia wakamwendea Daudi alipokuja na Wafilisti dhidi ya Sauli katika pambano. Lakini hawakuwasaidia Wafilisti kwasababu mabwana wa Wafilisti walishauriana na wakamfukuza Daudi. Walisema, “Atamwendea Bwana wake Sauli na kuhatarisha maisha yetu.”
20 Alipokwenda kwa Zikilagi, wanaume wa Manase walioungana nae walikuwa Adina, Yozabadi, Yediaeli, Yozabadi, Elihu, na Zilethai, viongozi wa maelfu wa Manase.
21 Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi, maana walikuwa wanaume wa mapambano. Baadae walikuwa wakuu katika jeshi.
22 Siku hadi siku, wanaume walikuja kwa Daudi kumsaidia, mpaka wakawa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
23 Hii ni kumbukumbu ya wanajeshi wa vita, walio kuja kwa Daudi Hebroni, kuupindua ufalme wa Sauli kwake, ilikutimiza neno la Yahweh.
24 Kutoka Yuda walio beba ngao na mkuki ni 6, 800, tayari kwa vita.
25 Kutoka kwa Wasimeoni walikuwa 7, 100 wanaume wa mapambano.
26 Kutoka kwa Walawi kulikuwa na wanaume wa mapambano 4, 600.
27 Yehoiada alikuwa kiongozi wa uzao wa Aruni, na kwa yeye walikuwa 3, 700.
28 Kwa Zadoki, kijana, mwenye nguvu, na mjasiri, walikuwa viongozi ishirini na mbili kwa familia ya baba yake.
29 Kutoka kwa Benjamini, kabila la Sauli, walikuwa elfu tatu. Wengi wao walibaki waaminifu kwa Sauli mpaka muda huu.
30 Kutoka kwa Waefraimu palikuwa na wanume wa mapambano 20, 800, wanaume maharufu kwenye familia za baba zao.
31 Kutoka kabila nusu la Manase palikuwa na wanaume elfu kumi na nane maharufu walio kuja kufanya Daudi mfalme.
32 Kutoka kwa Isakari, palikuwa na viongozi mia mbili walio kuwa na ufahamu wa nyakati na walijua nini Israeli ya paswa kufanya. Ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
33 Kutoka Zebuloni palikuwa na wanaume elfu hamsini wa mapambano, tayari kwa vita, na silaha zote za vita, na tayari kutoa uwaminifu usio pungua.
34 Kutoka kwa Naftali palikuwa na askari elfu moja, na pamoja nao wanaume elfu thelathini na saba wenye ngao na mikuki.
35 Kutoka kwa Wadani palikuwa na wanaume 28, 600 wameandaliwa kwa ajili ya pambano.
36 Kutoka kwa Asheri palikuwa na wanaume elfu arobaini wameandaliwa kwa pambano.
37 Kutoka upande wa pili wa Yordani, kutoka kwa Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase, palikuwa na wanaume 120, 000 wameandaliwa na silaha za kila namna kwa ajili ya pambano.
38 Wanajeshi hawa wote, waliandaliwa kwa pambano, kuja Hebroni kwa dhumuni maalumu la kumfanya Daudi mfalme wa Israeli yote. Israeli yote ilikubaliana na kumfanya Daudi mfalme.
39 Walikuwa na Daudi siku tatu, kula na kunywa, kwa kuwa ndugu zao waliwapa mahitaji ya kwenda nayo.
40 Kwa kuongezea, wao walio kuwa karibu nao, kwa umbali wa Isakari na Zebuloni na Naftali, walileta mkate kwa punda, ngamia, ng'ombe, na keki, mvinyo, mafuta, ng'ombe, na kondoo, kwa kuwa Israeli walikuwa wana sherehekea