14
1 Kisha Hiramu mfalme wa Tire alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, maseremala, na wajenzi. Walijenga nyumba kwa ajili yake.
2 Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli, na hivyo ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli
3 Ndani ya Yerusalemu, Daudi aliongeza wake, na akawa baba wa wana wengi na mabinti.
4 Haya yalikuwa majina ya watoto waliozaliwa nae huko yerusalemu: Shammua, Shobabu, nathani, Solimoni,
5 Ibhari, Elishama, Elpeleti,
6 Noga, Nefegi, Jafia,
7 Elishama, Beliada, na Elifeleti.
8 Sasa tangu Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo nae akaenda nje kinyume nao.
9 Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.
10 Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?” Yahweh akamwambia, “ Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako.”
11 Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, “ Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.” Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.
12 Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.
13 Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.
14 Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, “ Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.
15 Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti.”
16 Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.
17 Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.