25
1 Daudi na viongozi wa wafanyakazi wa hema la kuabudia walichaguliwa kwa kazi baadhi walikuwa wana wa Asafu, Hemani, na Yeduthuni. Wanaume hawa walitabiri kwa vinubi, vifaa vya uzi, na upatu. Hii ni orodha ya wanaume walioifanya hii kazi:
2 Kutoka wana wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania, na Asharela, wana wa Asafu, chini ya mwongozo wa Asafu, ambaye alitabiri chini ya uwangalizi wa mfalme.
3 Kutoka wana wa Yeduthuni: Gedalia, Zeri, Yeshaia, Shimei, Hashabia, na Matithia, sita kwa ujumla, chini ya mwongozo wa baba yao Yeduthuni, ambaye alipiga kinubi kwa kutoa shukurani na kumsifu Yahweh.
4 Kutoka wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na yerimothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti Ezeri, yoshibekasha, Mallothi, Hothiri, na Mahaziothi.
5 Hawa wote walikuwa wana wa Hemani mfalme wa manabii. Mungu alimpa Hemani wana kumi na nne na mabinti watatu kwa ajili ya kumpa heshima.
6 Hawa wote walikuwa chini ya mwongozo wa baba yao. Walikuwa ni waimbaji katika nyumba ya Yahweh, pamoja na upatu na vifaa vya uzi walivyohudumu katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni, na Hemani walikuwa chini ya uwangalizi wa mfalme.
7 Wao na kaka zao walikuwa na uwelewa na walifundishwa kutengeneza muziki kwa Yahweh walikuwa na idadi ya 288.
8 Walirusha kura kwa majukumu yao, wote sawa, sawa kwa vijana na kwa wazee, kwa walimua na kwa wanafunzi.
9 Sasa kuhusu wana wa Asafu: kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu; ya pili iliangukia katika familia ya Gedalia, idadi ya watu kumi na mbili;
10 ya tatu iliangukia kwa Zakuri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
11 ya nne iliangukia kwa Izri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
12 ya tano iliangukia kwa Nethania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
13 ya sita iliangukia kwa Bukia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
14 ya saba iliangukia kwa Yesharela, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
15 ya nane iliangukia kwa Yeshaia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
16 ya tisa iliangukia kwa Matania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
17 ya kumi iliangukia kwa Shimei, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
18 ya kumi na moja iliangukia kwa Azareli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
19 ya kumi na mbili iliangukia kwa Hashabia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
20 ya kumi na tatu iliangukia kwa Shubaeli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
21 ya kumi na nne iliangukia kwa Matithia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
22 ya kumi na tano iliangukia kwa Yeromothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
23 ya kumi na sita iliangukia kwa Hanania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
24 ya kumi na saba iliangukia kwa Yoshibekasha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
25 ya kumi na nane iliangukia kwa Hanani, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
26 ya kumi na tisa iliangukia kwa Malothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
27 ya ishirini iliangukia kwa Eliatha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
28 ya ishirini na moja iliangukia kwa Hothiri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
29 ya ishirini na mbili iliangukia kwa Gidalti, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
30 ya ishirini na tatu iliangukia kwa Mahaziothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
31 ya ishirini na nne iliangukia kwa Romamti Eza, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili.