29
1 Mfalme Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sulemani mwanangu, ambaye mwenyewe Mungu amemchagu, bado nimdogo na hana uzoefu, na jukumu ni kubwa. Maana hekalu sio kwa ajili ya watu bali la Mungu.
2 Hivyo nimefanya kwa ubora wangu kutoa kwa ajili ya hekalu la Mungu. Nina toa dhahabu kwa vitu vya kujengwa na dhahabu, fedha kwa vitu vya kujengwa na fedha, shaba kwa vitu vya kujengwa na shaba, nishati kwa vitu vya kujengwa na nishati, na mbao kwa vitu vya kujengwa na mbao. Pia nina toa mawe ya shohamu, mawe ya kupangwa, mawe ya upambaji wandani ya rangi mbali mbali - kila haina ya mawe ya thamani - na marimari kwa wingi.
3 Sasa, kwasababu ya mapenzi yangu kwa nyumba ya Mungu, Ninatoa hazina yangu binafsi ya dhahabu na fedha. Ninafanya hivi kwa nyongeza kwa yote niliyofanya katika hekalu takatifu:
4 talanta za dhahabu elfu tatu kutoka Ofiri, na talanta elfu saba za fedha zilizotakasika, ili kufunika kuta za majengo.
5 Ninachangia dhahabu kwa vitu vya kujengwa na dhahabu, na fedha kwa vitu vya kujengwa na fedha, na kazi zote zinazotakiwa kufanywa na wajenzi. Nani mwingine anataka kuchangia kwa Yahweh leo na kujitoa kwake?”
6 Kisha sadaka za hiari zilitolewa na viongozi wa mababu wa familia zao, viongozi wa makabila ya Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, na waamuzi waliojuu ya kazi ya mfalme.
7 Walitoa kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu talanta elfu tano na darkoni elfu kumi za dhahabu, talanta elfu kumi za fedha, talanta elfu nane za fedha, na talanta za chuma 100, 000.
8 Haao walio na mawe ya thamani waliyatoa katika Hazina ya nyumba Yahweh, chini ya usimamizi wa Yehieli, mzao wa Gerishoni.
9 Watu walifurahi kwa ajili ya hizi sadaka za hiari, kwasababu walitoa kwa moyo wao wote kwa Yahweh. Mfalme Daudi pia alifurahi sana.
10 Daudi alimbariki Yahweh mbele ya kusanyiko lote. Alisema, “Na uabudiwe, Yahweh, Mungu wa Israeli babu wetu, milele na milele.
11 Kwako, Yahweh, kuna ukuu, nguvu, utukufu, ushindi, na enzi. Kwa kuwa yote yalio mbinguni na duniani ni yako. Kwako ni ufalme, Yahweh, na umetukuzwa kama mtawala juu ya vyote.
12 Utajiri na heshima utoka kwako, unatawala juu ya watu wote. Mkononi mwako kuna nguvu na uwezo. Unao uweza na nguvu ya kuwafanya watu kuwa mkuu na kumpa uweza yeyote.
13 Kisha sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kusifu jina lako tukufu.
14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, tustahili kutoa kwa hiari hivi vitu? Kweli, vitu vyote vya toka kwako, na tumerudisha kwako vilivyo vyako.
15 Kwa kuwa sisi ni wageni na wasafiri mbele zako, mababu zetu wote walikuwa. Siku zetu katika dunia ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kubaki duniani.
16 Yahweh Mungu wetu, utajiri wote tulio kusanya kujenga hekalu kwa kuheshimu jina lako - watoka kwako na ni wako.
17 Ninajua, Mungu wangu, unachunguza moyo na wapendezwa na unyofu. Kwangu mimi, kwa unyofu wa moyo wangu nimetoa kwa hiari vitu vyote, na sasa natazama kwa furaha watu walio hapa wakitoa tunu kwako.
18 yahweh, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Israeli - mababu zetu - hifadhi hili katika fikra za watu wako. Elekeza mioyo yao kwako.
19 Mjalie Sulemani mwanangu moyo wa shauku wakutii amri zako, shuhuda za agano lako, na maagizo yako, na kutekeleza mipango hii yote ya kujenga nyumba niliyoiandaa.”
20 Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sasa mbariki Yahweh Mungu wenu.” Kusanyiko lote likambariki Yahweh, Munug wa mababu zao, wakainamisha vichwa vyao na kumuabudu Yahweh na kusujudu mbele za mfalme.
21 Kwa siku iliyo fuata, wakatoa dhabiu kwa Yahweh na kumtolea sadaka ya kuteketeza. Walitoa sadaka ya ng'ombe elfu moja, kondoo elfu moja, na wana kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji na dhabihu tele kwa Israeli yote.
22 Siku ile, walikunywa na kula mbele za Yahweh kwa furaha tele. Walimfanya Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme mara ya pili, na kumpaka mafuta ya mamlaka ya Yahweh kuwa mfalme. Pia walimpaka Zadoki mafuta kuwa mfalme.
23 Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha Yahweh kama mfalme baada ya Daudi baba yake. Alifanikiwa, na Israeli yote ikamtii.
24 Viongozi wote, wanajeshi, na Mfalme Daudi wanae wakaonyesha utii kwa Mfalme Sulemani.
25 Yahweh alimheshimu sana Sulemani na kumkirimia nguvu kubwa kuliko mfalme yeyote aliyetangulia kabla yake Israeli.
26 Daudi mwana wa Yese alitawala Israeli yote.
27 Daudi alikuwa mfalme wa Israeli kwa miaka arobaini. Alitawala kwa miaka saba Hebroni na miaka thelathini na tatu Yerusalemu.
28 Alikufa katika umri mzuri mkubwa, baada ya kufurahia maisha marefu, utajiri na heshima. Sulemani mwanae alitawala baada yake.
29 Mafanikio ya mfalme Daudi yameandikwa katika historia ya Samweli nabii, katika historia ya Nathani nabii, na katika historia ya Gadi nabii.
30 Yalio ekwa kwenye kumbukumbu ni matendo ya utawala wake, mafanikio yake na mambo yalio mdhuru, Israeli, na falme zote za nchi zingine.