13
1 Katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yeroboamu, Abiya akaanza kutawala juu ya Yuda.
2 Akatawala kwa miaka mitatu katika Yerusalemu; jina la mama yake aliitwa Maaka, binti wa Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
3 Abiya akaingia vitani na jeshi la askari, wenye nguvu, hodari, 400, 00 wanaume waliochaguliwa. Yeroboamu akapanga mistari ya vita dhidi yake yenye 800, 00 wanaume askari waliochaguliwa, wenye nguvu, hodari.
4 Abiya akasimama juu ya mlima Semaraimu, uliopo katika kilima cha nchi ya Efraimu, na akasema, “Nisikilizeni, Yeroboamu na Israeli wote!
5 Hamjui kwamba Yahwe, Mungu wa Israeli, alitoa sheria juu ya Israeli kwa Daudi milele, kwake na kwa wanaye kwa agano rasimi?
6 Bado Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumishi wa Selemani mwana wa Daudi, akainuka na kuasi dhidi ya bwana wake.
7 Watu wabaya, washirika wa karibu, wakamkusanyikia, wakamjia kinyume Rehoboamu mwana wa Selemani, wakati Rehoboamu alipokuwa mdogo na asiye na uzoefu na hakuweza kuwamudu.
8 Sasa mnasema kwamba mnaweza kuuzuia utawala wa Yahwe wenye nguvu katika mkono wa uzao wa Daudi. Ninyi ni jeshsi kubwa, na pamoja nanyi kuna ndama wa dhahabu ambao Yeroboamu alitengeneza kama miungu kwa ajili yenu.
9 Hamkuwafukuza nje makuhani wa Yahwe, uzao wa Haruni, na Walawi? Hamkujifanyia makuhani katika namna ya watu wa nchi zingine? Yeyote ajaye kujitakasa mwenyewe na ngo'mbe dume kijana, na madume ya kondoo anaweza kuwa kuhani wa kile ambacho siyo miungu.
10 Lakini kwetu, Yahwe ni Mungu wetu, na hatujamsahau. Tuna makuhani, uzao wa Haruni, wakimtumikia Yahwe, na Walawi, ambao wako kataika kazi yao.
11 Kila asubuhi na jioni humtolea Yahwe sadaka za kuteketezwa na uvumba mtamu. Pia hupanga mkate wa uwepo juu ya meza takatifu; pia huweka kinara cha dhahabu pamoaja na taa zake, ili watoe sadaka kila jioni. sisi huzishika sheria za Yahwe, Mungu wetu, Lakini ninyi mmemsahau.
12 Ona, Mungu yuko pamoja nasi katika vichwa vyetu, na makuhani wake wako hapa na tarumbeta kwa ajili ya kutoa sauti dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane na Yahwe, Mungu wa babu zenu, kwa maana hamtafanikiwa.”
13 Lakini Yeroboamu akaandaa mavamizi nyuma yao; jeshi lake lilikuwa mbele ya Yuda, na wavamizi nyuma yao.
14 Yuda walipoanagalia nyuma, tanzama, mapigano yalikuwa pote mbele na nyuma yao. Wakamlilia Yahwe kwa sauti, na makuhani wakayapuliza matarumbeta.
15 Kisha wanaume wa Yuda wakapiga kelele; walipopiga kele, ikawa kwamba Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.
16 Watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda, na akawatia kwenye mkono wa Yuda.
17 Abiya na jeshi lake wakawaua kwa mauji makuu; 500, 000 watu wanaume waliochaguliwa wa Israeli wakaanguka wamekufa.
18 Katika namna hii hii, watu wa Israeli wakatiishwa chini wakati huo, watu wa Yuda wakashinda kwa sababu walimtegemea Yahwe, Mungu wa babu zao.
19 Abiya akamshawishi Yeroboamu; akachukua miji kutoka kwake; Betheli pamoja na vijiji vyake, Yeshana pamoja na vijiji vyake, na Efroni pamoaaja na vijij vyake.
20 Yeroboamu hakupata naguvu tena katika siku za Abiya; Yahwe akampiga, na akafa.
21 Lakini Abiya akawa na nguvu sana; akachukua wanawake kumi na nne kwa ajili yake na akawa baba wa wana ishirini na mbili na mabinti kumi na sita.
22 Matendo ya Abiya yaliyosalia, tabia yake na maneno yake yameeandikwa katika kamusi ya nabii Ido.