17
1 Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoshafati akajiimarisha dhidi ya Israeli.
2 Akaweka majeshi katika miji yote Yuda yenye ngome, na akaweka magereza katika nchi ya Yuda na katika miji ya Efraimu, ambayo Asa baba yake alikuwa ameiteka.
3 Yahwe alikuwa pamoja na Yehoshafati kwa sababu alitembea katika njia za kwanza za baba yake Daudi, na hakuwatafuta Mabaali. (Baadhi ya mandiko ya kale hayana “Daudi”, na baadhi ya matoleo ya kisasa yameacha hili jina “Daudi).
4 Badala yake, alimtegemea Mungu wa baba yake, na alitembea katika amri zake, siyo katika tabia ya Israeli.
5 Kwa hiyo Yahwe akaimarisha sheria katika mkono wake; Yuda wote wakaleta kodi kwa Yehoshafati. Alikuwa na utajiri na heshima kubwa.
6 Moyo wake ulikuwa umejikita katika njia za Yahwe. Pia aliziondoa sehemu za juu na Maashera mbali na Yuda.
7 Katika mwaka wa tatu wa utawala wake aliwatuma wakuu wake Ben-haili, Obadia, Zekaria, Nethania, na Mikaya, ili wafundishe katika miji ya Yuda.
8 Pamoja nao walikuwepo Walawi: Shemaya, Nethanieli, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, na Tob-adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu.
9 Walifundisha katika Yuda, wakiwa na kitabau cha sheria ya Yahwe. Wakaenda karibu miji yote ya Yuda na kufundisha miongoni mwa watu.
10 Hofu ya Yahwe ikashuka juu ya falme zote za nchi, zilizouzunguka Yuda, kwa hiyo hazikufanya vita dhidi ya Yehoshafati.
11 Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi, fedha kama kodi. Waarabu pia wakamletea makundi, 7, 700 kondoo waume, na mbuzi 7, 770.
12 Yehoshafati akawa na nguvu sana.
13 Akajenga ngome na miji ya maghala katika Yuda. Alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda, na wanajeshsi—imara, wanaume hodari—katika Yerusalemu.
14 Hapa ni rodha yao, wamepangwa kwa majina ya nyumba za baba zo: Kutoka Yuda, maakida wa maelfu; Adna yule jemedari, na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 300, 000;
15 akifuatiwa na Yehonani jemedari, na pamoja naye wanaume 280, 00;
16 akifuatiwa na Amasia mwana wa Zikri, ambaye kwa hiari alijitoa kumtumikia Yahwe; na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 200, 000.
17 Kutoka Benyamini: Eliada mtu jasiri, na pamoja naye watu 200, 000 waliovaa upinde na ngao;
18 akifutiwa na Yehozabadi, na pamoja naye askari 180, 000 waliotayari kwa vita.
19 Hawa walikuwa ni wale ambao walimtumikia mfalme, miongoni mwao wale ambao mfalme aliwaweka katika miji ya ngome katika Yuda yote.