22
1 Wakaaji wa Yersusalemu wakamfanya Ahazia, mwana mdodgo wa Yehoramu, mfalme katika nafasi yake, kwa maana kundi la watu ambalo lilikuja na Waarabu katika ngome lilikuwa limewauwa wanaye wakubwa wote. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akawa mfalme.
2 Ahazia alikuwa na umri wa mika arobaini na mbili alipoanza kutawala; alitawala kwa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Athalia; alikuwa binti Omri.
3 Pia Ahazia alitembea katika njia za nyumba ya Ahabu kwa maana mama yake alikuwa mshauri katika kufanya mamabo maovu.
4 Ahazia alifanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama nyumba ya Ahabu walivyokuwa wakifanya, kwa maana walikuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hadi kuangamia kwake.
5 Pia aliufuata ushauri wao; akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu, huko Ramothi-gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.
6 Yoramu akaraudi Yezreeli kwa ajili ya kuponywa majeraha ambayo walipa huko Rama, alipopigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akaenda chini Yezreeli ili kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
7 Sasa uharibifu wa Ahazia ulikuwa umeletwa na Mungu kupitia kutembelewa na Yoramu. Alipokuwa amewasiri, alienda pamoja na Yeharamu ili kumvamia Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Yahwe alikuwa amemchagua kwa ajili ya kuingamiza nyumba ya Ahabu.
8 Ikawa kwamba, Yehu alikuwa akichukua hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu, kwamba aliwakuta viongozi wa Yuda na wana wa ndugu zake Ahazia wakimtumikia Ahazia. Yehu akawauwa.
9 Yehu akamtafuta Ahazia; Wakamkamata akiwa amejificha katika Samaraia, wakamleta kwa Yehu, na wakamuuwa. Kisha wakamzika, kwa maana walisema, “Ni mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Yahwe kwa moyo wake wote.” Kwa hiyo nyumba ya Ahazia haikuwa na nguvu zaidi kwa ajili ya kuutawala ule ufalme.
10 Sasa Athalia, mama wa Ahazia, akaoana kwamba mwanaye alikuwa amekufa, akaianuka na kuwauwa watoto wote wa kifalme katika nyumba ya Yehu.
11 Lakini Yehoshaba, binti wa mfalme, akamchukua Yoashi, mwana wa Ahazia, na akamvutia mbali kutoka miongoni mwa wana wa mfalme ambao waliuawa. Akamuweka yeye na mlezi wake katika chumba cha kulala. Kwa hiyo Yehoshaba, binti wa mfalme Yehoramu, mke wa Yehoiada kuhani (kwa maana alikuwa dada yake Ahazia), akamficha asimuone Athalia, kwa hiyo Athalia hakumuuwa.
12 Alikuwa pamoja nao, wakiwa wamejificha katika nyumba ya Mungu kwa miaka sita, Athalia alipotawala juu ya Yuda.