6
1 Basi sanduku la BWANA lilikaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba.
2 Ndipo Wafilisti wakawaita makuhani na waganga; wakawaambia, “Tulifanyie nini sanduku la BWANA? Twambieni jinsi ambavyo tunapaswa kulirudisha sanduku katika nchi yake.”
3 Makuhani na waganga wakasema, “Kama mtalirudisha sanduku la Mungu wa Israeli, msilipeleke bila zawadi; kwa namna yoyote ile mpelekeeni sadakaa ya hatia. Hapo ndipo mtapona, na mtajua ni kwanini mkono wake hadi sasa haujaondoka juu yenu.”
4 Ndipo wakawauliza, “Sadaka ya hatia itakuwa nini kwamba tunampelekea?” Wakawajibu, “Majipu matano ya dhahabu na panya watano wa dhahabu, Idadi hiyo ya watano ni sawa na idadi ya viongozi wa Wafilisti. Kwa sababu tauni ya aina moja iliwashambulia ninyi na viongozi wenu.
5 Kwa hiyo, nilazima mtengeneze mifano ya majipu yenu, na mifano ya panya wenu ambayo huiharibu nchi, na mpeni utukufu Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka juu yenu, kutoka juu ya miungu yenu, na kutoka juu ya nchi yenu.
6 Kwanini mfanye mioyo yenu kwa migumu, kama vile Wamisri na Farao walifanya mioyo yao kuwa migumu? Hicho ni kipindi ambacho Mungu wa Israeli aliwashughilikia sana; Je, Wamisri hawakuwaachilia watu, na wakaondoka?
7 Basi sasa, andaeni mkokoteni mpya pamoja na ng'ombe wawili wake wanaonyonyesha, ambao hawajawahi kufungwa nira. Wafungeni ng'ombe hao kwenye mkokoteni, lakini warudisheni wale ndama wao nyumbani.
8 Kisha lichukueni sanduku la BWANA na kuliweka ndani ya mkokoteni. Wekeni ndani ya kasha yale maumbo ya dhahabu mnayompelekea ambyo ni sadaka ya hatia kando yake. Ndipo mlipeleke lipate kuondoka.
9 Kisha muwe makini; kama litapanda kwenda kwa njia hadi nchini mwake hadi Beth Shemeshi, basi mjue kuwa BWANA ndiye aliyetenda pigo hili kubwa. Lakini kama halitakwenda, ndipo tutajua kwamba siyo mkono wake uliotupatia mateso; badala yake tutajua kuwa yaliyotupata ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu.
10 Watu hao wakafanya kama walivyoambiwa, walichukuwa ng'ombe wawili wanaonyonyesha, wakawafunga kwenye mkokoteni, na kuwabakiza ndama wao nyumbani.
11 Wakaliweka sanduku la BWANA juu ya mkokoteni, pamoja na lile kasha lililobeba panya wa dhahabu na yale maumbo ya majipu yao.
12 Hao ng'ombe waliondoka moja kwa moja kuelekea Beth Shemeshi. Walikwenda kwa kuifuata nija moja kuu, wakiteremka walipokuwa wakienda, na hwakugeuka upande wa kushoto au kulia. Viongozi wa Wafilisti walifuata kwa nyuma hadi mpaka wa Beth Shemeshi.
13 Nao watu wa Beth Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao katika bonde. Waliponyanyua macho yao juu na kuliona sanduku, wakafurahi.
14 Huo mkokoteni ulifikia ndani ya shamba la Yoshua wa Beth Shemeshi na ukasimama hapo. Kulikuapo jiwe kubwa mahali hapo, wakatayarisha kuni kutokana na mkokoteni huo, na wakawatoa ng'ombe hao kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya BWANA.
15 Walawi walilitelemsha sanduku la BWANA chini pamoja na kasha lake lililoyatunza yale maumbo ya dhahabu, wakaweka vitu hivyo juu ya hilo jiwe kubwa. Watu wa Beth Shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa na kutoa dhabihu kwa BWANA siku iyo hiyo.
16 Hao viongozi watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo.
17 Haya ndiyo majipu ya dhahabu ambayo Wafilisti walirudisha kama sadaka ya hatia kwa BWANA: moja kwa ajili ya Ashdodi, moja kwa Gaza, moja kwa Ashkeloni, moja kwa Gathi, na moja kwa Ekroni.
18 Idadi ya wale panya wa dhahabu ilikuwa sawa na ile ya idadi ya miji yote ya Wafilisti inayomilikiwa na viongozi watano, kwa miji iliyojengewa maboma na vijiji vya mashambani. Lile jiwe kubwa, ambalo kando yake waliweka sanduku la BWANA, lipo kama ushuhuda hadi leo katika shamba la Yoshua Mbeth- Shemeshi.
19 BWANA akawashambulia baadhi ya watu wa Bethi Shemeshi kwa sababu walichungulia ndani ya sanduku lake. Aliwaua watu sabini. Watu wakaomboleza, kwa sababu BWANA aliwapa watu pigo kubwa mno.
20 Watu wa Bethi Shemeshi wakasema, “Ni nani mwenye uwezo wa kushindana na BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na atampandia nani akitoka kwetu.”” Je, ni nani awezaye kusimama mbele ya BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na ni kwa nani ambako sanduku litaenda likitoka hapa.”
21 Wakawatuma wajumbe kwenda kwa wenyeji wa Kiriath Yearimu, wakisema, “Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; teremkeni na mkalipeleke kwenu.”